MHANDISI MRAMBA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MSUMBIJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 8, 2026

MHANDISI MRAMBA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MSUMBIJI


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Maputo, Msumbiji na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi, Tammy Kajigili.

Mhandisi Mramba ametembelea ubalozi huo akiwa nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Madini na Nishati 2026, uliohitimishwa tarehe 07 Mei 2026.

Mkutano huo ulijadili fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo barani Afrika hususani katika Sekta ya Nishati.

Katika Ofisi za Ubalozi huo Katibu Mkuu aliongozana na Khalifan Khalifan, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Petroli (PURA), Mha. Charles Sangweni, Mkurugenzi Mkuu wa PURA pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na PURA.

No comments:

Post a Comment