MRADI WA PAZA SAUTI+ WAENDESHA MAFUNZO DHIDI YA UKATILI SHINYANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 5, 2026

MRADI WA PAZA SAUTI+ WAENDESHA MAFUNZO DHIDI YA UKATILI SHINYANGA

 

 


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Stephen Magalla, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma za afya yaliyoandaliwa kwa lengo la kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na ukatili dhidi ya watoto (VAC) katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Stephen Magalla, akifungua mafunzo ya kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na ukatili dhidi ya watoto (VAC) kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Shinyanga.

**
Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na kwa ufadhili wa Sanlam Allianz, limeanza rasmi kuendesha mafunzo ya kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na ukatili dhidi ya watoto (VAC) katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Mafunzo haya yanatekelezwa kupitia Mradi wa Paza Sauti+ unaolenga kuiwezesha jamii kuzungumza wazi dhidi ya ukatili huku ukijenga uwezo wa watoa huduma za afya katika ukusanyaji na matumizi sahihi ya ushahidi wa kiforensiki.

Mradi wa Paza Sauti+ unalenga kuimarisha uwezo wa kiforensiki kwa uchunguzi unaotegemea ushahidi, kuhamasisha kutoa taarifa za matukio kwa wakati na kwa usalama, kuongeza uelewa wa umuhimu wa ushahidi wa vinasaba (DNA) katika upatikanaji wa haki na  kuimarisha uratibu kati ya sekta za afya, polisi na ustawi wa jamii.

Mafunzo kwa watoa huduma wa afya yanafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 7 Mei 2026, yakifuatiwa na mafunzo maalum kwa Wahudumu wa Afya ya Jamii (CHWs) tarehe 8 Mei 2026. 

Lengo ni kuimarisha mifumo ya utambuzi wa mapema, uripoti wa matukio, ukusanyaji wa ushahidi na utoaji wa huduma bora kwa manusura.

Kupitia mafunzo haya, washiriki wanapatiwa ujuzi wa kutambua matukio ya ukatili mapema
, Kuripoti kwa wakati na kwa usahihi, kukusanya na kuhifadhi ushahidi wa kiforensiki ipasavyo na kutoa huduma zinazomlenga manusura

Akizindua rasmi mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Stephen Magalla, amepongeza ushirikiano kati ya THPS, GCLA na Sanlam Allianz.

“Ushirikiano huu unaakisi mwitikio shirikishi unaohitajika katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto. Kuimarisha mifumo ya kiforensiki na uwezo wa watoa huduma kutaboresha kwa kiasi kikubwa msaada kwa manusura na kuhakikisha wanapata haki kwa wakati,” amesema  Magalla.

Kwa upande wake, Ndugu Julius Magabe, Mtendaji Mkuu wa Sanlam Allianz Life Insurance Tanzania, alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kuunga mkono mradi wa Paza Sauti+.

“Tunajivunia kuwa sehemu ya mradi huu muhimu. Tumeamua kuunga mkono Mradi wa Paza Sauti+ kama mchango wetu katika kupunguza na kupambana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto. Kama taasisi inayolinda maisha kupitia huduma za bima, tunatambua umuhimu wa kuunga mkono juhudi zinazolinda ustawi na heshima ya jamii.”

Washiriki wa mafunzo ni pamoja na watoa huduma za afya, maafisa wa dawati la jinsia kutoka Jeshi la Polisi, maafisa ustawi wa jamii na wadau wa kijamii. 

Mafunzo haya yanawawezesha kuimarisha mchango wao katika mnyororo mzima wa kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto, kuanzia utambuzi wa mapema hadi usimamizi wa kesi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa serikali wa ngazi ya mkoa, ukiashiria dhamira thabiti ya kisiasa na taasisi katika kukabiliana na vitendo vya ukatili na kuboresha upatikanaji wa haki kwa manusura.

Aidha, katika hafla hiyo walikuwepo pia Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (OC-CID) Kahama, SP Maro Kenyunko, pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Abrahamani Kibakaya, ambao wameipongeza THPS, GCLA na Sanlam Allianz kwa hatua za wakati muafaka katika kuziba mapengo yaliyopo kwenye kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kupitia Mradi wa Paza Sauti+.

Wadau wamebainisha changamoto zinazoendelea katika ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kiforensiki, hali inayochangia kuchelewesha au kudhoofisha mashauri ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto. 

Mradi huu unalenga kuziba mapengo hayo kwa kujenga uwezo wa kitaalamu na kuongeza uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa kuripoti mapema.

Mradi wa Paza Sauti+ unatekelezwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama na Kituo cha Afya Nyasubi, ukihusisha kata za Nyasubi na Malunga, ukiendana na Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (NPA-VAWC II).

Kwa kuimarisha mifumo na ushiriki wa jamii, Mradi wa Paza Sauti+ unalenga kuhakikisha manusura wanasikilizwa, wanapatiwa huduma bora kwa wakati, na wanapata haki stahiki.

THPS pia inaipongeza Sanlam Allianz kwa mchango wake katika kupambana na ukatili kupitia programu za uwajibikaji kwa jamii.

Kuhusu THPS

Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa nchini, linalojikita katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya na ustawi wa jamii kwa Watanzania wote. Tangu mwaka 2011, THPS imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania kuimarisha mifumo ya afya na jamii kupitia mbinu mbalimbali zinazotegemea Ushahidi wa kisayansi.

Kuhusu Paza Sauti+

Mradi wa Paza Sauti+ ni mpango unaoshirikisha Serikali na sekta binafsi unaolenga kuimarisha sauti za jamii, kujenga uwezo wa taasisi, na kuboresha upatikanaji wa haki kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Stephen Magalla, akifungua mafunzo ya kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na ukatili dhidi ya watoto (VAC) kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Stephen Magalla, akifungua mafunzo ya kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na ukatili dhidi ya watoto (VAC) kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Shinyanga.
Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Dkt. Baraka Msumi akizungumza kwenye mafunzo ya kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na ukatili dhidi ya watoto (VAC) kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Shinyanga.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (OC-CID) Kahama, SP Maro Kenyunko  akizungumza kwenye mafunzo ya kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na ukatili dhidi ya watoto (VAC) kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Shinyanga.
Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mohamed Mdemu akizungumza kwenye mafunzo ya kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na ukatili dhidi ya watoto (VAC) kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Shinyanga.
Mratibu wa Mradi wa Paza Sauti + kutoka Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), Agnes Kirato akielezea mradi wa Paza Sauti +
Mratibu wa Mradi wa Paza Sauti + kutoka Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), Agnes Kirato akielezea mradi wa Paza Sauti +
Mratibu wa Mradi wa Paza Sauti + kutoka Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), Agnes Kirato akielezea mradi wa Paza Sauti +


No comments:

Post a Comment