TANZANIA YASISITIZA USHIRIKIANO KIKANDA KUONGEZA THAMANI ALMASI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 20, 2026

TANZANIA YASISITIZA USHIRIKIANO KIKANDA KUONGEZA THAMANI ALMASI



Na Mwandishi Wetu, Freetown- Sierra Leone


Tanzania imesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Kikanda katika kuongeza thamani Madini ya Almasi, uwazi katika usimamizi wa rasilimali madini na kuimarisha mchango wa Sekta ya Madini katika maendeleo ya uchumi wa nchi wanachama Zinazozalisha Madini ya Almasi Afrika (ADPA).

Hayo yalibainishwa Mei 19, 2026 mjini Freetown, Sierra Leone, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki katika Mkutano wa 11 wa Kawaida wa Kamati ya Wataalam wa umoja huo.

Mkutano huo unawakutanisha wataalam kutoka nchi wanachama wa ADPA kujadili masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha usimamizi, biashara na maendeleo ya sekta ya almasi barani Afrika.

Aidha, katika mkutano huo, wajumbe walijadili taarifa ya mwaka ya Mkurugenzi Mtendaji wa ADPA ya mwaka 2025, utekelezaji wa bajeti na taarifa za fedha za mwaka 2025 pamoja na taarifa ya ukaguzi wa nje wa hesabu kwa kipindi cha 2023–2024.

 Aidha, masuala ya msamaha wa madeni, daftari la hatari, maendeleo ya uwezo wa taasisi na uanachama wa ADPA katika Shirika la Viwango Duniani (ISO) yalipata nafasi ya kujadiliwa kwa lengo la kuimarisha ufanisi wa taasisi hiyo.

Vilevile, mkutano ulipokea taarifa za maendeleo kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Almasi na maadhimisho ya miaka 20 ya ADPA, mapitio ya mkakati wa mawasiliano na masoko, utekelezaji wa ukaguzi wa ndani wa miaka 2023–2025 pamoja na mapendekezo ya sera ya usimamizi wa utendaji kazi.


No comments:

Post a Comment