VIWANJA 16 VITAKAVYOTUMIKA KWENYE KOMBE LA DUNIA 2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 27, 2026

VIWANJA 16 VITAKAVYOTUMIKA KWENYE KOMBE LA DUNIA 2026


Mashindano ya Kombe la Dunia 2026 yanatarajiwa kuanza Juni 11,2026 na kuwa ya kihistoria baada ya FIFA kuthibitisha kuwa mechi zote zitachezwa katika viwanja 16 vilivyopo kwenye mataifa matatu ambayo ni Marekani, Mexico na Canada.

Mashindano hayo yatakuwa ya kwanza kushirikisha mataifa matatu kama wenyeji wa pamoja huku yakitarajiwa kuwa na jumla ya mechi 104 kutokana na kuongezwa kwa idadi ya timu zitakazoshiriki kutoka 32 hadi 48.

Nchini Marekani, viwanja 11 vitatumika ambapo miongoni mwa viwanja vikubwa ni MetLife Stadium lenye uwezo wa kuchukua mashabiki 82,500 na litakaloandaa mechi nane ikiwemo fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Pia AT&T Stadium lenye uwezo wa mashabiki 94,000 litakuwa miongoni mwa viwanja vikubwa zaidi katika mashindano hayo huku likitarajiwa kuandaa mechi tisa.

Viwanja vingine vya Marekani ni Mercedes-Benz Stadium (75,000), SoFi Stadium (70,000), Levi's Stadium (71,000), Lumen Field (69,000), Hard Rock Stadium (65,000), NRG Stadium (72,000), Arrowhead Stadium (73,000), Lincoln Financial Field (69,000) pamoja na Gillette Stadium lenye uwezo wa mashabiki 65,000.

Kwa upande wa Mexico, viwanja vitatu vitatumika ambapo maarufu zaidi ni Estadio Azteca lenye uwezo wa mashabiki 83,000 ambalo pia litatumika kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo.

Viwanja vingine vya Mexico ni Estadio Akron lenye uwezo wa mashabiki 48,000 pamoja na Estadio BBVA lenye uwezo wa mashabiki 53,500.

Nchini Canada, viwanja viwili vimeteuliwa ambavyo ni BC Place lenye uwezo wa mashabiki 54,500 litakaloandaa mechi saba pamoja na BMO Field lenye uwezo wa mashabiki 45,500 litakaloandaa mechi sita.

Kwa mujibu wa ratiba ya FIFA, baadhi ya viwanja vitakuwa na michezo kati ya sita hadi tisa huku Marekani ikipewa idadi kubwa ya mechi kutokana na kuwa na viwanja vingi zaidi vya kisasa vitakavyotumika katika mashindano hayo makubwa duniani.














No comments:

Post a Comment