Watumishi wa Wizara ya Ujenzi, leo Mei 01, 2026, wameungana na wafanyakazi wengine katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kudumisha juhudi, mshikamano na uzalendo katika kulijenga Taifa.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa Jamhuri, yakianza na maandamano eneo la Bunge hadi uwanjani jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule.
Maadhimisho ya mwaka huu yanabebwa na Kauli Mbiu:
"Kazi zenye staha ni nguzo imara kwa maendeleo endelevu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050".









No comments:
Post a Comment