CP MKAMA: WANANCHI TOENI USHIRIKIANO KWA POLISI KATA KUKOMESHA UHALIFU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 15, 2026

CP MKAMA: WANANCHI TOENI USHIRIKIANO KWA POLISI KATA KUKOMESHA UHALIFU


Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Alex Mkama, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi Kata katika maeneo yao ili kubaini na kuzuia uhalifu kabla haujatokea.

CP Mkama ametoa wito huo Juni 15, 2026, katika kikao na askari wa Mkoa wa Dodoma kilicholenga kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi na kujadili mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoikabili jamii.

Amesema Jeshi la Polisi limeendelea kusogeza huduma karibu na wananchi kupitia mfumo wa Polisi Kata, hivyo ni muhimu kwa jamii kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kushiriki katika vikundi vya ulinzi shirikishi na kutoa taarifa za uhalifu pamoja na wahalifu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wakati.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gallus Hyera, amewasisitiza askari wa mkoa huo kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uzalendo, sambamba na kutoa elimu ya ulinzi na usalama kwa wananchi ili kuimarisha ushirikiano na kukemea vitendo vya uhalifu katika jamii.

No comments:

Post a Comment