DCP NGOSO, DCF NGENYA NA DCI MWAIFUGE WAJIONEA HUDUMA NA SHUGHULI ZA UREKEBISHAJI KATIKA BANDA LA MAGEREZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 17, 2026

DCP NGOSO, DCF NGENYA NA DCI MWAIFUGE WAJIONEA HUDUMA NA SHUGHULI ZA UREKEBISHAJI KATIKA BANDA LA MAGEREZA


Na. Ssgt Mawazo Mtondo - Dodoma.


Mkuu wa Sehemu ya Usimamizi wa Maadili na Ushughulikiaji wa Malalamiko (Mrejesho) wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolphina Ngoso, Mkuu wa Kitengo cha Utumishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Naibu Kamishna wa Zimamoto na Uokoaji (DCP) Fatma Ngenya na Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Bahati Mwaifuge kwa nyakati tofauti, leo Juni 17, 2026 wametembelea Banda la Maonesho la Jeshi la Magereza lililopo katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Viongozi hao walifanya ziara hiyo katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayoendelea kufanyika Jijini Dodoma, ambapo walipata fursa ya kujionea huduma mbalimbali, shughuli za urekebishaji wa wafungwa, pamoja na kazi za uzalishaji mali zinazotekelezwa na Jeshi la Magereza kupitia Programu mbalimbali za urekebishaji.

Kwa nyakati tofauti, wageni hao walipokelewa na Mkuu na Msemaji wa Jeshi la Magereza katika Maonesho ya Mwaka huu, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Elmas L.Mgimwa, ambaye aliwaeleza majukumu ya Jeshi la Magereza katika Usalama, mchango wake katika utoaji wa huduma za urekebishaji na mageuzi yaliyopo sasa katika utekelezaji wa majukumu yake yanayochsngia kwa kiasi kikubwa maendeleo nch kijamii na kiuchumi.

No comments:

Post a Comment