DKT. NCHIMBI ATEMBELEA BANDA LA TANESCO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 5, 2026

DKT. NCHIMBI ATEMBELEA BANDA LA TANESCO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametembelea banda la Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) kwenye kilele cha Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika jijini Dodoma.

Mhe. Balozi Dkt. Nchimbi ametembelea banda la hilo leo Juni 5, 2026 ambapo amepata nafasi ya kuelezwa miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ikiwemo matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa umeme pamoja na utunzaji wa mazingira kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme.

Akitoa maelezo kwa Mhe.Balozi Dkt.Nchimbi Mkuu wa Kitengo cha Mazingira Wizara ya Nishati Emmilian Nyanda ameeleza kuwa TANESCO imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kutoa elimu ya umuhimu wa Nishati Safi ya kupikia kwa Umeme kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anashiriki kwenye suala la utunzaji wa Mazingira.

Maonesho ya mwaka ya mazingira 2026 yalikuwa na kauli mbiu isemayo Dira 2050, Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.

No comments:

Post a Comment