EWURA CCC YAWASHAURI WATUMIAJI WA GESI KUTUMIA MIZANI ILI KUPATA UJAZO SAHIHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 23, 2026

EWURA CCC YAWASHAURI WATUMIAJI WA GESI KUTUMIA MIZANI ILI KUPATA UJAZO SAHIHI



Na Boniphace John -Dodoma


BARAZA la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji (EWURA CCC) limewashauri watumiaji wa gesi kupima mitungi  ya gesi kwa kutumia mzani ili kupata ujazo sahihi.


Akizungumza na waandishi wa habari  Afisa huduma kwa wateja Mwandamizi EWURA CCC Mkoa wa Dodoma, Amani Mbogo katika maadhimisho ya kitaifa ya wiki ya utumishi wa Umma 2026 yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali Park vilivyopo Jijini Dodoma leo hii juni 23,2026 amesema yapo malalamiko mbalimbali yanayotokana na gesi pamoja na umeme kuisha haraka hivyo BARAZA  lipo kwaajili ya kumlinda na kumtetea mtumiaji anayetumia huduma za nishati na maji.


Amesema Kupitia banda la EWURA CCC watumiaji zaidi ya 500 wameweza kufika katika banda na kutoa maoni yao,malalamiko na ushauri kuhusu huduma za nishati na maji.


"Kupitia haya maadhimisho watumiaji wengi wamejifunza kwamba unapokwenda kununua mtungi wa gesi hakikisha unaupima kwa kutumia mzani kupata ujazo sahihi ili kuendana na thamani ya pesa halisi uliyoitoa,"

Aidha Ameendelea kusema Malalamiko mengi yametolewa na kupokelewa  ikiwemo changamoto za kutokupatikana kwa maji,umeme kuisha haraka ndani ya nyumba.


"Moja ya ushauri tuliyowapa ni kuhakikisha wanatumia fundi mwenye leseni ya EWURA kwasababu moja ya kazi za EWURA  ni kutoa leseni kwa mafundi wa umeme.


"Unakuta mteja anaweza akawa amemchukua fundi ambaye hana leseni na nyumba yake ikapata shida mwisho wa siku atakimbilia EWURA CCC lakini atakosa msaada kwasababu alichukua fundi ambaye hatambuliki,"amesema Mbogo.


Hata hivyo amesema wanaahidi kuendelea kushughulikia malalamiko vilevile kutoa ushauri na kuelimisha watu waweze kujua huduma za nishati na maji zikoje.


Nao Baadhi  ya wananchi walio pata wasaa wakutembelea banda hilo wameonyesha kufurahishwa na huduma hizo  zinazotolewa na EWURA CCC.


Toster Cyprian ambaye ni mkazi wa mtaa wa chimuli kata ya  makole mkoani Dodoma amesema alikuwa na changamoto nyingi ikiwemo ya maji taka ambapo kwa muda mrefu hakujuwa pakuiwasilisha changamoto yake lakini baadaa ya kufika banda la  EWURA CCC  ameweza kupata elimu nakufahamu pakuiwasilisha changamoto yake kwaajili ya ufumbuzi.


Pia amewaomba wananchi  kuwa na desturi ya kuhudhuria kwenye maonyesho pindi yanapo tokea kwaajili ya kuweza kupata elimu  ya vitu mbalimbali .




No comments:

Post a Comment