Meneja wa kampasi ya Dodoma ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Epaphra Manamba amesema katika kuendana na mahitaji ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 IAA itaendelea kuwekeza katika mitaala itakayojikita kwenye elimu – ujuzi (Competence based ) na ubunifu ili kuwaandaa wataalam watakaokuwa na uwajibikaji jumuishi katika kujenga Uchumi Jumuishi.
Prof. Manamba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la IAA kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
“Dira ya Taifa ya 2050 imeipa sekta binafsi nafasi kubwa, tunapoongelea uwajibikaji jumuishi na uchumi jumuishi sekta binafsi inahusika kwa asilimia 100;sekta binafsi imepewa nguvu kwa sababu maendeleo ya nchi hii yatachangiwa na sekta binafsi na serikali itaandaa miundombinu ili kuiwezesha sekta binafsi kufanya kazi yake”
“Kozi za IAA zinamuandaa mwanafunzi si tu kwamba aende akaajiriwe bali aweze kujiajiri na kuajiri wengine.IAA ina Kiotamizi (Incubator) kazi yake ni kuwasaidia wanafunzi kuandaa mawazo ya biashara, kusimamia waweze kusajili biashara na kampuni zao, kuwaunganisha na wadau, wafadhili wakiwa bado chuoni; wengi wao wamefanikiwa kumaliza masomo yao tayari wakiwa wanamiliki kampuni zao na wanajipatia kipato,” amesema Prof. Manamba.
Mhitimu wa IAA ngazi ya Shaahda na Shahada ya Uzamili Bw. Justine Kitaja,amesema anajivunia kuwa sehemu ya mafaniko ya IAA anaipongeza IAA kwa ubinifu katika kuandaa mitaala yao na kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora inayoendana na mahitaji ambayo inawasaidia katika maeneo wanayofanyia kazi.











No comments:
Post a Comment