Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Kikundi cha Kigamboni Vijana Unity kutoka Mtaa wa Kigamboni, Kata ya Kikuyu Kaskazini kimekabidhiwa Bajaji tano kupitia mkopo usio na riba wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia Benki ya NMB ili kukiwezesha kikundi kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika viunga vya Manispaa ya zamani jijini hapa, Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Amos Mubusi alisema kuwa benki hiyo inaendelea kushirikiana na serikali katika kuwawezesha vijana na makundi maalum ili kukuza biashara na kuongeza ushiriki wao katika uchumi.
Mubusi alisema kuwa Benki ya NMB imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa vikundi 304 nchini, wakati Halmashauri ya Jiji la Dodoma, vikundi 19 vikipatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 228.
Aidha, aliwataka wanachama wa Kigamboni Vijana Unity kutumia fursa hiyo kwa uwazi, nidhamu na uaminifu ili kuhakikisha mradi huo unaleta mafanikio yaliyokusudiwa na kuwa mfano kwa vijana wengine.
Kwa upande wake Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, CPA. David Rubibira alieleza kuwa uwezeshaji huo ni sehemu ya jitihada za serikali za kuwawezesha vijana kujiajiri na kuongeza kipato chao kupitia shughuli halali za kiuchumi.
Alisema kuwa halmashauri itandelea kutoa mikopo hiyo ya asilimia 10 kupitia mapato yake ya ndani ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika nayo.
Nae Afisa Mtendaji Mtaa wa Kigamboni, Farijala Kunga alisema kuwa kikundi hicho ni cha mfano kwa mtaa wake. “Sisi viongozi wa mtaa, tulikitembelea kikundi na kukipatia elimu ya matumizi sahihi ya mkopo waliopata ili waweze kukuwa zaidi kiuchumi.

Aidha, tuliwashauri mkufuata sharia za usalama barabarani kwa kipindi chote pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo” alisema Kunga.
Kikundi cha Kigamboni Vijana Unity kinatajwa kuwa kikundi cha mfano katika Mtaa wa Kigamboni kimekabidhiwa Bajaji tano zenye thamani ya shilingi milioni 60 fedha ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

No comments:
Post a Comment