MATUKIO KATIKA PICHA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA PD-MIS DAR ES SALAAM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 10, 2026

MATUKIO KATIKA PICHA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA PD-MIS DAR ES SALAAM


Na Mwandishi wetu


Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Ayoub Kibao ametoa rai kwa washiriki mafunzo ya ukusanyaji, uhifadhi na usimamizi wa taarifa sahihi za wenye ulemavu kufanya kazi hiyo kwa weledi ili kusaidia Serikali kuhakikisha inaendelea kuweka mipango ya kuhakikisha kundi la wenye ulemavu linahudumiwa ipasavyo.

Dkt. Kibao ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo hayo leo tarehe 10/06/2026 akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abdul Rajabu Mhinte. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maafisa Ustawi wa Jamii pamoja na Maafisa TEHAMA kutoka halmashauri mbalimbali za Mkoa Dar es salaaam ili kusaidia kuimarisha matumizi ya mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi na usimamizi wa taarifa sahihi za watu wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment