MIKOA YAANZA KUSHINDANA UMITASHUMTA 2026 IRINGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 8, 2026

MIKOA YAANZA KUSHINDANA UMITASHUMTA 2026 IRINGA


OWM-TAMISEMI, Iringa


Wanafunzi kutoka Mikoa 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar wameanza kushindana katika Mashindano ya Umoja na Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) yanayofanyika Kitaifa Mkoani Iringa.

Michezo hiyo ambayo imenza leo tarehe 8 Juni 2026, inachezwa katika viwanja vya shule ya Sekondari Iringa Wasichana, Chuo cha Ualimu Kleruu, Kichangani na Shule ya Sekondari Lugalo.

Michezo inayoshindaniwa kwa Vavulana na Wasichana ni pamoja na Soka, Riadha, mpira wa Kikapu, Netiboli,Mpira wa Mikono,Meza na Kriketi.

Aidha Mashindano hayo pia yanawajumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao wanashinda katika Soka,Riadha na mpira wa Goli (Goal Ball) ambao ni mahususi kwa ajili ya wenye uono hafifu.

Vilevile mikoa itashindana kwenye Sanaa za Maonesho zitakazojumuisha Kwaya, Ngoma za Asili na Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flavor).

UMITASHUMTA & UMISSETA 2026 inaandaliwa na kuratibiwa na OWM-TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa na kaulimbiu isemayo "Michezo na Sanaa Shuleni Daraja la Ajira, Afya na Ushindani wa Kimataifa"

No comments:

Post a Comment