Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo leo Juni 8, 2026 ameshiriki Ufunguzi wa Jukwaa la Utalii, Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri linalofanyika jijini Cairo, likiwakutanisha viongozi wa Serikali, taasisi za utalii, wafanyabiashara, wawekezaji na wadau mbalimbali kutoka nchi hizo mbili kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kukuza fursa za biashara, uwekezaji na utalii.
Jukwaa hilo limeandaliwa chini ya kaulimbiu inayohamasisha uhusiano kati ya Bahari ya Mediterania na Bahari ya Hindi kupitia masoko, utalii, biashara na uwekezaji, likitoa fursa kwa wadau kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano yenye manufaa kwa pande zote mbili.
Aidha, washiriki walipata fursa ya kushuhudia video mbalimbali za kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na kufanya mikutano ya kibiashara (B2B) na majadiliano yaliyolenga kuanzisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa sekta binafsi kutoka Tanzania na Misri.
Jukwaa hilo limehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi , Naibu Waziri wa Utalii na Mambo Kale Misri, Mhe. Yomna El Bahar, Balozi wa Tanzania nchini Misri Meja Jenerali Richard Makanzo na viongozi wengine mbalimbali wa Serikali kutoka nchi zote mbili.











No comments:
Post a Comment