SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA GAMIS KUIMARISHA USIMAMIZI WA MALI ZA UMMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 13, 2026

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA GAMIS KUIMARISHA USIMAMIZI WA MALI ZA UMMA


Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi. Pili Mnyema, akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli wa Taasisi za Umma kutoka Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Idara zinazojitegemea na taasisi nyingine zinazofunga hesabu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro, iliyofanyikia katika ukumbi wa ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi. Pili Mnyema, akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Mali za Serikali Bw. Ismael Ogaga, wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli wa Taasisi za Umma kutoka Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Idara zinazojitegemea na taasisi nyingine zinazofunga hesabu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro, iliyofanyikia katika ukumbi wa ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani.

Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Mali za Serikali Bw. Ismael Ogaga, akifafanua jambo wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli kuhusu matumizi bora ya mali za Serikali, usimamizi wa ajali na potevu za mali za umma na mwongozo wa kushughulikia madai ya fidia pamoja na usimamizi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mali (GAMIS), yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani.

Msimamizi wa Mali za Serikali Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Neema Luanga, akifanya wasilisho kuhusu majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali na upungufu wa Taasisi za Umma kwenye Usimamizi wa Mali, wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli wa Taasisi za Umma kutoka Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Idara zinazojitegemea na taasisi nyingine zinazofunga hesabu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro, iliyofanyikia katika ukumbi wa ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Bahati Geuzye, akiuliza swali wakati wa wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli wa Taasisi za Umma kutoka Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Idara zinazojitegemea na taasisi nyingine zinazofunga hesabu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro, yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani.

Baadhi ya Maafisa Masuuli wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli ikiwemo majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali na Upungufu wa Taasisi za Umma kwenye usimamizi wa mali, usimamizi wa vifaa vya kuhifadhia fedha, mali za thamani na nyaraka muhimu, usimamizi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mali (GAMIS),usimamizi wa ajali na potevu za mali za umma na mwongozo wa kushughulikia madai ya fidia pamoja, yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Dkt. Revocatus Mushumbusi, akiuliza swali wakati wa Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli wa Taasisi za Umma kutoka Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Idara zinazojitegemea na taasisi nyingine zinazofunga hesabu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro, yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani.

Meza Kuu ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi. Pili Mnyema (katikati), Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali Wizara ya Fedha Bw. Ismael Ogaga (kulia) na Msimamizi wa Mali za Serikali Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Farida Chamkwea (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Sektretarieti baada ya kuhitimishwa kwa Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro, yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Pwani)


Na. Josephine Majura, WF, PWANI


Serikali imezitaka taasisi zote za umma nchini kuimarisha usimamizi wa mali za Serikali kwa kuhakikisha taarifa zote za mali zinaingizwa na kutunzwa katika Mfumo wa Serikali wa Usimamizi wa Mali (GAMIS), ili kuongeza uwajibikaji, kuimarisha matumizi ya rasilimali za umma na kupunguza hoja za ukaguzi.

Maagizo hayo yametolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi. Pili Mnyema, wakati akifungua Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli wa Taasisi za Umma kutoka Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Idara zinazojitegemea na taasisi nyingine zinazofunga hesabu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro, yaliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoani Pwani .

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Bi. Mnyema alisema mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wakuu wa taasisi za umma katika kusimamia mali za Serikali kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Fedha za Umma Sura ya 348, Kanuni za Usimamizi wa Mali za Umma za mwaka 2024 pamoja na miongozo mbalimbali inayosimamia eneo hilo.

“Mali za umma ni rasilimali muhimu zinazowezesha Serikali kutoa huduma kwa wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo, huku wastani wa asilimia 70 ya bajeti za taasisi za umma ukitumika katika ununuzi unaozalisha mali hizo, usimamizi wake unapaswa kuzingatia uwajibikaji, ufanisi na utii wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa”,alisema Bi. Mnyema.

Aidha, taasisi hizo zimetakiwa kuhakikisha mali chakavu, sinzia, ziada na zilizokwisha muda wa matumizi zinaondoshwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo kabla ya Septemba 30, 2026 ili kuimarisha ufanisi wa matumizi ya mali za umma.

Katika hatua nyingine Bi. Mnyema, amezitaka taasisi za umma kuwasilisha taarifa za ajali, hasara na upotevu wa mali kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali ndani ya siku 30 tangu tukio litokee na mali zilizopata ajali au uharibifu zifanyiwe matengenezo mara baada ya kupata kibali husika.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Mali za Serikali Bw. Ismael Ogaga, alisema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa mahsusi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usimamizi wa mali za Serikali.

Alifafanua kuwa kupitia mafunzo hayo, washiriki wamepata uelewa wa kina kuhusu sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa mali za umma, jambo litakalosaidia kuimarisha uwajibikaji, kuongeza ufanisi wa matumizi ya rasilimali za Serikali na kupunguza hoja za ukaguzi.

Aidha, alisema Wizara ya Fedha itaendelea kutoa mafunzo hayo katika mikoa yote nchini ili kuhakikisha watumishi wa umma wanapata maarifa na stadi zinazohitajika katika kusimamia mali za Serikali.

Kwa upande wao mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Dkt. Revocatus Mushumbusi, alisema kuwa watahakikisha wanayafanyia kazi yote waliyojifunza ili kuimarisha usimamizi wa mali za umma katika taasisi zao.

Aidha, aliiomba Wizara ya Fedha kuendelea kutoa mafunzo kama hayo kwa watumishi wa ngazi za chini wanaoshiriki moja kwa moja katika shughuli za usimamizi wa mali, ili kuongeza uelewa na kuhakikisha utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu unafanyika kwa ufanisi katika ngazi zote.

Katika mafunzo hayo jumla ya mada sita ziliwasilishwa ikiwemo majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali na Upungufu wa Taasisi za Umma kwenye usimamizi wa mali, usimamizi wa vifaa vya kuhifadhia fedha, mali za thamani na nyaraka muhimu, usimamizi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mali (GAMIS), usimamizi wa ajali na potevu za mali za umma na mwongozo wa kushughulikia madai ya fidia pamoja.


Hadi sasa Wizara ya Fedha imeshafanya mafunzo hayo kwa Maafisa Masuuli katika Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Pwani.

No comments:

Post a Comment