TBS YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA IMANI YA WALAJI NA KUKUZA VIWANDA VYA NDANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 6, 2026

TBS YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA IMANI YA WALAJI NA KUKUZA VIWANDA VYA NDANI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb) amelitaja Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwa ni nguzo kuu ya kulinda afya za walaji na kuchochea ustawi wa viwanda nchini.

Amebainisha hayo Katika hafla maalum ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Shirika hilo pamoja na Utoaji wa Tuzo kwa watumishi wa sasa na wastaafu kwa kutambua mchango wao uliojenga misingi imara ya udhibiti wa ubora Juni 6,2026, Jijini Dar es Salam.

Mhe. Londo Mhe.Londo amebainisha kuwa Kutokana na kukua kwa kasi kwa uwekezaji katika sekta za viwanda, kilimo, madini, na nishati, kuna uhitaji wa uwepo wa mifumo thabiti ya uhakiki wa ubora ili kulinda soko la ndani hivyo Kupitia huduma zake za upimaji na utoaji wa alama za ubora, TBS imekuwa chachu ya kukuza viwanda vya ndani na kuongeza imani ya walaji, jambo linaloiwezesha Tanzania kunufaika kikamilifu na fursa za masoko makubwa ikiwemo Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA).

Aidha alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kukuza uchumi kupitia maboresho ya miundombinu ya usafirishaji, nishati, na mifumo ya kidijitali na ameeleza kuwa maboresho ya sera na sheria yanalenga kuvutia uwekezaji na kuimarisha sekta binafsi, huku akiiasa TBS kuhakikisha kuwa ongezeko la uzalishaji nchini linaenda sambamba na uzingatiaji wa viwango vinavyotambulika duniani.

Akiangazia mustakabali wa miaka 50 ijayo, Mhe. Londo alieleza kuwa dunia inabadilika kwa kasi kiteknolojia na kiushindani, hivyo kuna mahitaji makubwa ya kuwa na TBS ya kisasa inayoendeshwa kwa maarifa hivyo Shirika hilo limetakiwa kuwekeza kwenye maabara zenye vifaa vya kisasa zaidi, kuongeza wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu, na kuimarisha mifumo ya kidijitali yenye ufanisi ili kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na ubunifu duniani.

Mkakati huo wa kuimarisha mifumo ya viwango unaelezwa kuwa msingi imara wa kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kisasa, jumuishi, na unaotegemea uzalishaji wenye thamani kubwa. Mhe. Londo aliongeza kuwa kusimamiwa vyema kwa usalama na ubora wa bidhaa kutasababisha bidhaa na huduma za Kitanzania kukubalika kwa urahisi katika soko la kimataifa na kikanda.

Vile vile Naibu Waziri alitoa rai kwa sekta binafsi, wazalishaji, na wafanyabiashara kuendelea kushirikiana kwa karibu na TBS ili kujenga utamaduni endelevu wa uzingatiaji viwango na uzalishaji wenye tija.

No comments:

Post a Comment