TIMU YA OFISI YA RAIS–UTUMISHI YAKAGUA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 25, 2026

TIMU YA OFISI YA RAIS–UTUMISHI YAKAGUA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI DODOMA




Na Antonia Mbwambo - Dodoma



Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais–UTUMISHI kwa kushirikiana na Watumishi Housing Investment imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi awamu ya pili katika Wilaya ya Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia ubora, thamani ya fedha na ratiba iliyopangwa.

Ziara hiyo imeongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute, ambaye amesema Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya kazi na makazi ya watumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bw. Allute amesisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa miradi, matumizi sahihi ya rasilimali za umma na ukamilishaji wa kazi kwa wakati huku viwango vya ubora vikizingatiwa.

Aidha, ametoa maelekezo kwa wasimamizi wa miradi na wakandarasi kushughulikia kwa haraka changamoto zilizobainika ili kuhakikisha malengo ya miradi hiyo yanafikiwa kama ilivyopangwa.

Ziara hiyo imekuwa sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha uwekezaji unaofanywa unaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa manufaa ya watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla.

Katika ukaguzi huo, timu imetembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika Kituo cha Afya Hombolo, Shule ya Sekondari Mtemichiloloma, Kituo cha Afya Mkonze na Shule ya Sekondari Bihawana, ambapo imejionea maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo na imefanya majadiliano na wasimamizi pamoja na wakandarasi kuhusu hatua zilizofikiwa na changamoto zinazojitokeza.



No comments:

Post a Comment