ALLIANCE LIFE YAZIDI KUPANUA WIGO WAKE. YAFUNGUWA OFISI DODOMA , WANANCHI WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 1, 2026

ALLIANCE LIFE YAZIDI KUPANUA WIGO WAKE. YAFUNGUWA OFISI DODOMA , WANANCHI WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA


Na Boniphace John -Dodoma.

‎Sekta ya bima nchini imeendelea kuonyesha ukuaji mkubwa huku Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ikitaja kuongezeka kwa matumizi ya bima kutaiwezesha sekta hiyo kufikia lengo la kuchangia asilimia tatu ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2030. 

‎Hayo yamesemwa Juni 30, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mauzo ya Alliance Life.


‎Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware, Meneja wa Mipango na Utafiti wa TIRA,Bw. Edgar Shao, amesema soko la bima nchini limeendelea kukua na mamlaka imeendelea kusimamia mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma za bima na sekta hiyo inaongeza mchango wake katika uchumi wa taifa.

‎Amesema TIRA imeipongeza Alliance Life kwa kufungua ofisi ya mauzo jijini Dodoma, akieleza kuwa hatua hiyo imeendelea kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwapa fursa ya kupata ushauri na huduma za bima kwa urahisi zaidi. 

‎" mamlaka imeendelea kuwahimiza wananchi wa Dodoma kutumia fursa hiyo kwa kutembelea ofisi za Alliance ili kujipatia huduma mbalimbali zikiwemo bima za maisha, bima za vyombo vya moto, bima za kilimo na bidhaa nyingine za bima ambazo zimeendelea kuwa muhimu katika kulinda maisha na mali," amesisitiza shao.


‎Aidha, amesema mchango wa sekta ya bima katika Pato la Taifa umefikia asilimia 2.18 mwaka huu, jambo ambalo limeonyesha kuwa sekta imeendelea kupiga hatua kuelekea lengo la Serikali la kufikia asilimia tatu mwaka 2030. 


‎Nae  Mkuu wa Kitengo cha Bancassurance wa Alliance Life, Bi.Tumaini Pyanisa, amesema kampuni hiyo imefungua ofisi ya mauzo Dodoma kwa lengo la kuhakikisha huduma za bima ya maisha zimeendelea kuwafikia Watanzania popote walipo. Amesema Alliance Life imekuwa kampuni ya kwanza ya bima ya maisha kuwa na ofisi ya mauzo katika mkoa wa Dodoma.

‎Pyanisa amesema kampuni hiyo imeendelea kuongozwa na kaulimbiu ya "Ukifikiria maisha, fikiria Alliance," akieleza kuwa imeendelea kuweka thamani na kipaumbele kwa maisha ya kila Mtanzania kupitia huduma zake za bima ya maisha.

‎"Alliance Life imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima za maisha, huku ikishirikiana na taasisi za kifedha,taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, shule na waajiri ili kuhakikisha huduma hizo zinawafikia wananchi wengi zaidi. Amesema mwitikio wa wateja umeendelea kuongezeka kadri elimu hiyo inavyoendelea kutolewa.

‎"bima za maisha zimeendelea kutoa kinga ya kifedha pale mteja anapofiwa na ndugu wa karibu, anapopata ulemavu wa kudumu au anapokumbwa na changamoto nyingine zinazoathiri maisha yake. Hivyo, amewahimiza Watanzania, hususan wakazi wa Dodoma, kujitokeza kukata bima ili kujilinda wao na familia zao pamoja na kuchangia ukuaji wa sekta ya bima nchini,"amesema pynisa.


Alliance life ,wateja ndio kipaumbele na huduma zinazo faa huongeza thamani ya maisha .





No comments:

Post a Comment