FURSA 40 ZA MAFUNZO YA UYAYA QATAR ZATANGAZWA KWA WATANZANIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 27, 2026

FURSA 40 ZA MAFUNZO YA UYAYA QATAR ZATANGAZWA KWA WATANZANIA



Na Mwandishi Wetu | Dodoma


Watanzania 40 wenye sifa wamepata nafasi ya kujiunga na mafunzo ya uyaya nchini Qatar kupitia ushirikiano wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Wakala wa Almaha Travel and Tours Company Limited pamoja na Khalid Islamic Foundation.

Mafunzo hayo yatadumu kwa miezi 12 na yatatoa fursa ya ajira kwa wahitimu watakaofanikiwa kuyakamilisha.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa Julai 27, 2026, waombaji wanapaswa kuwa wanawake wenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 40, wawe na elimu ya sekondari au Thanawi, wajue kuzungumza na kuandika lugha ya Kiarabu pamoja na kuwa na maadili mema. Mafunzo hayo yatafanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Uyaya nchini Qatar (Qatar Nanny Academy).

Tangazo hilo linaeleza kuwa gharama zote za mafunzo, matibabu, visa, tiketi ya ndege, malazi na chakula zitalipiwa na chuo husika.

Aidha, washiriki watapatiwa posho ya kujikimu ya Riyal 500 za Qatar kila mwezi, sawa na takribani Shilingi 360,000 za Kitanzania, huku wahitimu wakitarajiwa kupewa ajira nchini Qatar kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuhitimu.

Maombi yanapokelewa kuanzia Julai 27 hadi Julai 31, 2026, huku usaili ukitarajiwa kufanyika Agosti 3, 2026 jijini Dar es Salaam. Waombaji wa nje ya Dar es Salaam watafanya usaili kwa njia ya mtandao.

Baada ya kutuma maombi kupitia anuani zilizotajwa kwenye tangazo, waombaji wanapaswa pia kujisajili kupitia mfumo wa ajira wa Serikali.

No comments:

Post a Comment