MPOTO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI SABASABA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 7, 2026

MPOTO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI SABASABA


Msanii maarufu wa sanaa za maonesho na mashairi, Mrisho Mpoto ni miongoni mwa wananchi wanaoendelea kutembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda hilo, Mjomba amepata elimu kuhusu Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024–2034 unaolenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Pia ameelezwa kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na faida zake katika kulinda afya, mazingira na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

No comments:

Post a Comment