SERIKALI YASISITIZA UTAFITI WA DAWA ZA ASILI KUFANYIKA NDANI YA NCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 8, 2026

SERIKALI YASISITIZA UTAFITI WA DAWA ZA ASILI KUFANYIKA NDANI YA NCHI


Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema itaendelea kuweka msukumo katika kuendeleza sayansi na teknolojia kwani ndiyo msingi wa kukuza uchumi kupitia maarifa na kuboresha huduma katika sekta mbalimbali.

Akizungumza Julai 8, 2026, baada ya kutembelea Taasisi ya Afya na Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute-IHI), tawi la Bagamoyo mkoani Pwani, Prof. Mkenda amesema taasisi hiyo ni ya mfano katika tafiti za kisayansi ambazo zinasaidia maendeleo ya sekta ya afya.

Amepongeza kazi za Taasisi hiyo akitolea mfano utafiti chanjo za malaria, majaribio ya dawa (clinical trials) na teknolojia za kisasa zinazotumika katika utafiti.

Mkenda amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa IHI na vyuo vikuu vya ndani na vya kimataifa ili kuijengea Tanzania yenye uwezo wa kufanya tafiti zenye viwango vya kimataifa, kuzalisha maarifa na bidhaa zenye manufaa kwa wananchi.

Prof. Mkenda ameongeza kuwa serikali inataka kuona dawa za asili zikifanyiwa utafiti, majaribio ya awali (_pre-clinical_) na _clinical trials_ ili kuthibitisha ubora na usalama wake hapa hapa nchini, hatua itakayowezesha Tanzania kuzalisha dawa zilizotokana na gunduzi za ndani na kunufaika na matokeo yake kwa kuwa na haki miliki.

Aidha, amesema wizara inaendelea kupitia sera ya Sayansi na Teknolojia ili kuhakikisha inakuwa shirikishi, inatekelezeka na inapimika, sambamba na kuvitaka vyuo vikuu nchini kuwekeza kwa uzito sawa katika ufundishaji na utafiti.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendahi wa Taasisi ya Afya na Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute-IHI), tawi la Bagamoyo Dkt Ally Olotu amesema taasisi hiyo immejikita katika kuleta mabadiliko katika mifumo ya afya nchini na nje ya mipaka, kufanya tafiti za chanjo mbalimbali na tabia za jamii kuhusiana na Afya.

No comments:

Post a Comment