VIFARANGA VYA SAMAKI MILIONI 1.5 VYAPANDIKIZWA ZIWA RWAKAJUNJU - KARAGWE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 24, 2026

VIFARANGA VYA SAMAKI MILIONI 1.5 VYAPANDIKIZWA ZIWA RWAKAJUNJU - KARAGWE


Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwawezesha wananchi wa Wilaya ya Karagwe kuanza kunufaika na uchumi wa buluu kupitia zoezi la upandikizaji wa vifaranga milioni 1.5 vya samaki aina ya sato katika Ziwa Rwakajunju lililopo wilayani Karagwe.

Bashungwa ametoa shukrani hizo leo, tarehe 23 Julai 2026, katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la upandikizaji wa vifaranga vya samaki katika Ziwa Rwakajunju, iliyofanyika Kijiji cha Kafunjo, Kata ya Kamagambo, Wilaya ya Karagwe.


Bashungwa ameeleza kuwa zoezi la upandikizaji wa vifaranga linaenda kuleta mageuzi makubwa kwa wananchi na ameiomba Serikali kuongeza vifaranga vya samaki kufikia milioni 5 pamoja na boti ya kufanya doria katika ziwa hilo.

Aidha, ili kuendelea kusimamia kikamilifu rasilimali hiyo, Mbunge Bashungwa ameahidi kumpatia pikipiki Afisa Uvuvi wa Kata, ambayo itamwezesha kutekeleza majukumu yake ya usimamizi na ufuatiliaji.

Awali, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Nazael Madalla ameeleza kuwa Serikali itaongeza vifaranga katika Ziwa Rwakajunju pamoja na kufanya upimaji wa ziwa hilo ili kubaini kama linafaa kwa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mhe. Zaituni Msogfe ameishukuru Serikali kwa kuleta vifaranga milioni 1.5 vyenye thamani ya shilingi milioni 450.

No comments:

Post a Comment