HATUA MOJA, OKOA MAISHA: MANYARA YALENGA SH1.5 BILIONI KWA WATOTO NJITI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, August 22, 2026

HATUA MOJA, OKOA MAISHA: MANYARA YALENGA SH1.5 BILIONI KWA WATOTO NJITI

Na Mwandishi Wetu, Manyara

MBIO za hisani za Manyara Tanzanite Marathon 2026 zimefanyika leo katika Mji wa Babati, mkoani Manyara, huku waandaaji wakiwa na lengo la kukusanya Sh1.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi na uwezeshaji wa wodi maalum ya kuwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

Mbio hizo zilizoendeshwa chini ya kaulimbiu “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto Njiti”, zimewakutanisha wananchi, wanariadha na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini, kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya kwa watoto wachanga na watoto njiti.

Mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mwigulu Nchemba, ambaye ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Daniel Sillo, amepongeza Mkoa wa Manyara kwa kuanzisha mbio hizo, akisema ni ubunifu unaolenga kushirikisha jamii katika kuchangia huduma za afya.

Sillo amesema Manyara Tanzanite Marathon ni mfano wa namna matukio ya michezo yanavyoweza kutumika katika kuhamasisha jamii na wadau kuchangia miradi yenye manufaa kwa wananchi, hususan katika sekta ya afya.

Amesema jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono na maeneo mengine nchini ili kuongeza ushiriki wa jamii katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jafari Rajabu, amesema mbio hizo zina umuhimu mkubwa katika juhudi za kuokoa maisha ya watoto, huku akiwataka wananchi na wadau kuendelea kuunga mkono mipango inayolenga kuboresha huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amewashukuru wadau walioshiriki katika maandalizi na utekelezaji wa mbio hizo, akisema ushirikiano wao umewezesha kufanikisha tukio hilo lenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wanaohitaji huduma maalumu za afya.
Sendiga amesema fedha zitakazopatikana kupitia mbio hizo zitaelekezwa katika kufanikisha ujenzi na uwezeshaji wa wodi maalum kwa ajili ya kuwahudumia watoto njiti, ambao huhitaji huduma za kitaalamu na vifaa maalumu tangu wanapozaliwa.

Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wamesema walishiriki si kwa ajili ya mazoezi na afya zao pekee, bali pia kuchangia juhudi za kuokoa maisha ya watoto wachanga na watoto njiti.

Wamesema Manyara Tanzanite Marathon imewapa fursa ya kuunganisha michezo na shughuli za kijamii, huku wakitoa wito kwa wananchi wengine kushiriki katika matukio yenye malengo ya kuboresha afya na ustawi wa jamii.

Manyara Tanzanite Marathon 2026 imeweka lengo la kukusanya Sh1.5 bilioni, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto Njiti” inayolenga kuongeza uwezo wa huduma za afya kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment