Na Boniphace John – Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Bi. Jenifa Christian Omolo, amesema Serikali itaendelea kuweka sera, mifumo, rasilimali na mazingira wezeshi kwa vijana kupitia programu na fursa mbalimbali, ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, mikopo inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri, fursa za manunuzi ya umma, programu za kukuza ujuzi pamoja na uwezeshaji katika sekta za uzalishaji.
Amesema hatua hizo zinalenga kuhakikisha vijana wanapata fursa za kujikwamua kiuchumi, kujenga maisha bora na kuondokana na kukata tamaa pamoja na msongo wa mawazo unaoweza kusababishwa na changamoto za maisha.
Bi. Omolo amesema kijana anayelenga kujikwamua kiuchumi na kujenga maendeleo yake hapaswi kutegemea matumaini pekee, bali anapaswa kujipanga, kujifunza, kusikiliza ushauri, kujitambua, kuwa na nidhamu na kuchukua hatua.
“Matumaini pekee hayatoshi. Kijana anapaswa kujipanga, kujifunza, kusikiliza ushauri, kujitambua, kuwa na nidhamu na kuchukua hatua ili kufikia malengo yake,” amesema.
Amesisitiza kuwa kukutana na changamoto au kufanya makosa katika maisha hakumaanishi kuwa huo ndiyo mwisho wa safari kwa kijana, bali ni sehemu ya kujifunza, kujitathmini na kufanya maboresho katika maeneo ambayo amekosea.
Bi. Omolo ameyasema hayo Agosti 11, 2026, wakati akifungua Kongamano la Vijana lililofanyika Nzuguni jijini Dodoma, lililolenga kuchochea fikra, ubunifu na matumizi ya fursa miongoni mwa vijana, pamoja na kutoa nafasi ya kujadili changamoto na maeneo mbalimbali yanayogusa maisha na maendeleo yao.
Amesema kongamano hilo linajadili maeneo manne muhimu, ambayo ni ajira na kazi zenye staha; afya na ustawi wa vijana; ubunifu na uchumi wa kidijitali; pamoja na elimu ya uraia, uzalendo na ushiriki wa vijana katika maendeleo.
Kwa mujibu wa Bi. Omolo, maeneo hayo yana umuhimu mkubwa katika kumjenga kijana mwenye ujuzi, afya njema, maadili, uwezo wa kutumia teknolojia na utayari wa kushiriki katika kutatua changamoto zinazolikabili jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha, ameeleza kuwa kongamano hilo linapaswa kuchochea hatua za vitendo, ili kila kijana anayeshiriki aweze kuondoka akiwa amejifunza jambo jipya, kuboresha ujuzi wake, kujenga tabia chanya, kutambua matumizi sahihi ya teknolojia na kuongeza ushiriki wake katika maendeleo ya jamii na taifa.
Amesema ushiriki wa vijana katika majukwaa kama hayo ni muhimu kwa kuwa unawapa nafasi ya kujadili changamoto zao, kubadilishana uzoefu na kutambua fursa zinazoweza kuwasaidia kujenga maisha yenye tija na kuchangia maendeleo ya taifa.

No comments:
Post a Comment