SERIKALI YAWEKEZA BILIONI 16 ZA PAMPU RUVU JUU KUONGEZA UHAKIKA WA MAJI DAR NA PWANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, August 30, 2026

SERIKALI YAWEKEZA BILIONI 16 ZA PAMPU RUVU JUU KUONGEZA UHAKIKA WA MAJI DAR NA PWANI


Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewekeza kiasi cha Shilingi bilioni 16 za pampu mpya nane katika Mtambo wa Uzalishaji Maji Ruvu wa Juu, ili kuongeza uwezo wa uzalishaji na usafirishaji wa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.

Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mazingira na Maji, ikiongizwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Jackson Kiswaga (Mb), imejionea uwekezaji huo katika mtambo eneo la Mlandizi, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, amesema pampu sita kati ya nane tayari zimewasili, na saba zikipangwa kufungwa Ruvu Juu.

Pampu hizo zina uwezo wa kusafirisha kati ya lita milioni 1.5 hadi 2 kwa saa, ikilinganishwa na pampu za awali zilizokuwa na uwezo wa kusafirisha lita 900,000 hadi milioni moja kwa saa.

Mhe. Kiswaga amesema Kamati imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha miundombinu ya maji, akibainisha kuwa kukamilika kwa ufungaji wa pampu hizo kutaongeza ufanisi wa utoaji wa huduma.

Ufungaji wa pampu zilizobaki unaendelea, na kazi zinafanyika kwa utaratibu unaolenga kutohatarisha huduma ya maji kwa wananchi.Serikali yawekeza Bilioni 16 za pampu Ruvu juu kuongeza uhakika wa maji Dar na Pwani Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewekeza kiasi cha Shilingi bilioni 16 za pampu mpya nane katika Mtambo wa Uzalishaji Maji Ruvu wa Juu, ili kuongeza uwezo wa uzalishaji na usafirishaji wa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani. Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mazingira na Maji, ikiongizwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Jackson Kiswaga (Mb), imejionea uwekezaji huo katika mtambo eneo la Mlandizi, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki. Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, amesema pampu sita kati ya nane tayari zimewasili, na saba zikipangwa kufungwa Ruvu Juu. Pampu hizo zina uwezo wa kusafirisha kati ya lita milioni 1.5 hadi 2 kwa saa, ikilinganishwa na pampu za awali zilizokuwa na uwezo wa kusafirisha lita 900,000 hadi milioni moja kwa saa. Mhe. Kiswaga amesema Kamati imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha miundombinu ya maji, akibainisha kuwa kukamilika kwa ufungaji wa pampu hizo kutaongeza ufanisi wa utoaji wa huduma. Ufungaji wa pampu zilizobaki unaendelea, na kazi zinafanyika kwa utaratibu unaolenga kutohatarisha huduma ya maji kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment