TAKUKURU YAKABIDHI VIFAA MUHIMU VYA WATOTO WACHANGA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA -BOMBO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, August 16, 2026

TAKUKURU YAKABIDHI VIFAA MUHIMU VYA WATOTO WACHANGA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA -BOMBO





TAASISI ya Kuzuia na Kupambana ana Rushwa nchini (TAKUKURU) imekabidhi vifaa muhimu vya kisasa kwa ajili ya kuimarisha huduma kwa watoto wachanga hususani waliozaliwa kabla ya wakati (njiti) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo.


Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Leo Agosti 15,2026 imepokea vifaa muhimu vya kisasa kwa ajili ya kuimarisha huduma kwa watoto wachanga, hususan waliozaliwa kabla ya wakati.

Vifaa hivyo, ambavyo ni Phototherapy na Infant Warmer, vimetolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini-TAKUKURU ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Hospitali ya Bombo katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Akikabidhi vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika Hospitalini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini, Bw. Crispin Chalamila, amesema taasisi hiyo imeamua kutoa msaada huo baada ya kuona juhudi zinazofanywa na Hospitali ya Bombo katika kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Tanga wanapata huduma bora za afya.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo, Dkt. Husein Mangaa, ameishukuru TAKUKURU kwa msaada huo wa thamani kubwa na kwamba vitaongeza uwezo wa hospitali katika kutoa huduma kwa watoto wachanga wanaohitaji uangalizi maalum.

Naye Daktari Bingwa wa Watoto, Dkt. Mohamed Saleh, ameipongeza TAKUKURU kwa kuunga mkono juhudi za hospitali, akieleza kuwa vifaa hivyo vitasaidia wataalam kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kwa watoto wachanga.

Uongozi wa Hospitali ya Bombo umeeleza kuwa upatikanaji wa vifaa hivyo ni hatua nyingine muhimu katika kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto na kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga na maeneo jirani.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tanga, Dadi Kolimba ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tanga na viongozi kutoka timu ya Afya ya mkoa wa Tanga ikiongozwa na Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Bwana Imani Clemence.













No comments:

Post a Comment