VIONGOZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAFANYA 'ROYAL TOUR' HIFADHI YA TAIFA NYERERE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 4, 2026

VIONGOZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAFANYA 'ROYAL TOUR' HIFADHI YA TAIFA NYERERE

Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo, Agosti 4, 2026, wamehitimisha Mkutano wao wa Kimkakati (Retreat) kwa kufanya ziara maalumu ya kutembelea vivutio vya utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa Nyerere kupitia Game Drive na utalii wa boti, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi.

Akizungumza mara baada ya Ziara hiyo Dkt. Abbasi amesema ziara hiyo imewapa viongozi fursa ya kujionea kwa karibu utajiri wa vivutio vya utalii pamoja na shughuli za uhifadhi zinazoendelea ndani ya hifadhi hiyo, ambayo ndiyo kubwa zaidi nchini Tanzania.

“Tumeshuhudia wanyamapori mbalimbali wakiwemo swala, twiga, tandala mkubwa, viboko, nyani na aina nyingi za ndege wanaopatikana katika mfumo wa ikolojia wa hifadhi hii ya Nyerere,” amesema Dkt. Abbasi.

Ameongeza kuwa Hifadhi ya Taifa Nyerere imeendelea kuwa moja ya vivutio vikubwa vya utalii barani Afrika, ikiwa na wanyama adimu kama mbwa mwitu wa Afrika (African wild dogs), pamoja na mandhari ya kuvutia ya maziwa matano yanayochangia kwa kiasi kikubwa uhifadhi wa viumbe hai.

Ziara hiyo inaakisi dhamira ya Wizara ya kuendelea kuimarisha uhifadhi wa maliasili na kukuza utalii endelevu, sekta inayochangia kwa kiwango kikubwa uchumi wa Taifa.

No comments:

Post a Comment