WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA WAPATIWA ELIMU YA KINGA NA UTAMBUZI WA SARATANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 10, 2026

WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA WAPATIWA ELIMU YA KINGA NA UTAMBUZI WA SARATANI

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, akizungumza katika zoezi la utoaji wa elimu kuhusu saratani pamoja na vipimo vya uchunguzi wa awali wa saratani kwa watumishi wa wizara hiyo, linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.
Afisa Utumishi Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Salum Said, akifafanua jambo katika zoezi la utoaji wa elimu kuhusu saratani pamoja na vipimo vya uchunguzi wa awali wa saratani kwa watumishi wa Wizara hiyo, linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.
Daktari Bingwa wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Frank Ruta, akitoa elimu kuhusu kinga, utambuzi na matibabu ya saratani kwa watumishi wa Wizara ya Fedha, katika zoezi linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha wakifuatilia elimu iliyokuwa inatolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, kuhusu namna ya kujikinga, kutambua dalili za awali na kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na ugonjwa wa saratani, katika zoezi linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

Na. Jordan Mbwambo, WF, Dodoma.


Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road imeanza kutekeleza zoezi la utoaji wa elimu kuhusu saratani pamoja na vipimo vya uchunguzi wa awali wa saratani kwa watumishi wa Wizara hiyo ili kuongeza uelewa wa namna ya kujikinga, kutambua dalili za awali na kuchukua hatua stahiki kukabiliana na ugonjwa huo.

Zoezi hilo litakalohusisha utoaji wa elimu kuhusu saratani mbalimbali, ikiwemo saratani ya matiti, tezi dume na shingo ya kizazi, pamoja na vipimo vya awali linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, alisema ni muhimu kwa watumishi kufuatilia elimu ya afya ya saratani ili kuwa na uelewa wa kutosha kukabiliana na ugonjwa huo.

‘‘Ni muhimu kuwa na uelewa sahihi kuhusu saratani, hususan kwa kuzingatia kwamba utambuzi wa ugonjwa huo katika hatua za awali una nafasi kubwa katika matibabu na kuokoa maisha’’’ Alisema Bw. Sendo.

Aliwasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kutumia fursa hiyo kupata elimu pamoja na kufanya vipimo vya awali vinavyotolewa ili kufahamu hali zao za afya.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Saratani, Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Frank Ruta, aliwahimiza watumishi hao kutopuuza mabadiliko au dalili zisizo za kawaida katika miili yao na kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya uchunguzi na ushauri wa kitaalamu.

Alisema utambuzi wa saratani katika hatua za awali unaongeza nafasi ya mafanikio ya matibabu, hivyo jamii inapaswa kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara na kuchukua hatua za mapema katika kuzuia na kukabiliana na saratani.

Dkt. Ruta alisemna elimu hiyo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uelewa wa watumishi na jamii kwa ujumla kuhusu afya na kuwahamasisha kuchukua hatua za mapema katika kuzuia na kukabiliana na saratani.

No comments:

Post a Comment