BAHI KIJANI CUP KUWA FURSA KUCHOCHEA UCHUMI WA VIJANA BAHI -CDE SANGULAH - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 2, 2026

BAHI KIJANI CUP KUWA FURSA KUCHOCHEA UCHUMI WA VIJANA BAHI -CDE SANGULAH


Na Mwandishi wetu - Dodoma.


Mashindano ya Bahi Kijani Cup 2026 yanatarajiwa kuanza rasmi   jumapili septemba 6, 2026, kwa mchezo wa ufunguzi utakaowakutanisha magwiji wa soka Bahi  na Ilindi  kwenye Uwanja wa Bahi sokoni  kuanzia saa 10 jioni.


Kabla ya kuanza kwa mchezo huo kutafuatia na sherehe za uzinduzi (Burudani) ambapo wasananii  mbalimbali  watasherehesha.


Mashindano hayo yanayotajwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kwani  yameanzishwa kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vya soka kwa vijana,kutoa fursa ya viongozi  kukutana na vijana na kusikiliza changamoto zao na kisha kuziwasilisha kwenye mamlaka husika  kwaajili ya utatuzi ,halikazarika kuimarisha mshikamano wa jamii pamoja na kuhamasisha maendeleo ya michezo katika wilaya  ya Bahi .


Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma, mwenyekiti wa jumuiya ya  umoja wa vijana  wa CCM  wilaya ya Bahi Justine Lucas Sangulah  amesema maandalizi yote ya ligi hiyo yamekamilika kinacho subiriwa ni kuanza kwa mtanange wa kumpata mshindi  huku akibainisha mpaka sasa timu 24 kutoka  kata 22 za Bahi zenye jumla ya  vijiji 59  na vitongoji zaidi ya 500 zimejisajili  kuwa tayari kwa mwandindano.


Bahi kijani  Cup 2026 itazikutanisha timu mbalimbali kutoka kata tofauti za jimbo hilo, huku zikitarajiwa kuonyesha ushindani mkubwa katika kuwania ubingwa wa mashindano hayo kutokana na zawadi  Nono zilizowekwa na waandaaji  kwa mshindi wa kwanza, wapili na watatu .


“mauli mbiu ya Bahi  Kijani Cup ni VIJANA 

NA FURSA, TUNAONGEZA TABASAMU” na hii imedhihirika kwa vitendo kwani zawadi zilizoandaliwa kwa washindi ni kama ifuatavyo,mshindi wa kwanza atapewa pair ya ngombe wa maksai (ng’ombe wawili wa kulima) 

jembe la kuvutwa na ng’ombe na joki lake kwa maana hawa washindi tayari tutawasaidia kutengeneza kikundi na tayari wataenda kulima na kufanya  shughuli zingine za kijamii, kadhali mshindi wa pili tutampatia mbuzi wawili na mshindi wa tatumbuzi mmoja, hivyo itoshe tu kusema hii sioya kukosa",. amesema.


aidha Sangulah amebainisha wadau watakao hudhuria katika hafra ya  uzinduzi huo akiwataja Ofisi ya Maendeleo ya jamii Kutoka Halmashauri  huku  akimtaja Mgeni rasmi atake Fungua mashindano hayo  ambae ni MNEC  na Katibu wa UVCCM Taifa  Halid Mwinyi .


amesema Baada ya mchezo wa ufunguzi, ratiba ya michezo mingine itaendelea kama ilivyopangwa na waandaaji, huku timu zikitarajiwa kuendelea kushindana katika hatua za awali.


Wananchi wa Bahi na maeneo ya jirani wamealikwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo hiyo na kuwa sehemu ya mafanikio ya Bahi kijani  Cup 2026.

No comments:

Post a Comment