TANESCO YAKAMATA WATEJA WALIOCHEPUSHA UMEME - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 2, 2026

TANESCO YAKAMATA WATEJA WALIOCHEPUSHA UMEME

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ubungo jijini Dar es Salaam limeendelea na operesheni yake maalum ya kuwabaini na kuwachukulia hatua wateja ambao wanatumia umeme bila kulipia wakiwa wameunganishiwa umeme na vishoka mtaani kinyume na utaratibu.

Katika operesheni hiyo TANESCO Mkoa wa Ubungo imekamata baadhi ya wateja wake katika maeneo ya Mabibo External,Mburahati na Kimara Kilungure na miongoni mwa wateja hao wamekuwa wakitumia umeme wa TANESCO bila kulipia kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Akizungumza leo Septemba 2,2026 wakati wa operesheni hiyo fundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ubungo Salum Bure amesema wamewakamata wateja ambao wamechepusha umeme kupitia vishoka.

“Katika eneo la Mtaa wa Amani uliopo Mabibo External kuna mteja tumekuta amechepusha umeme na mara ya mwisho amenunua umeme Agosti mwaka 2025.Hivyo kwa zaidi ya mwaka mmoja halipi umeme na ameunganishiwa na kishoka.

“Pia katika Mtaa wa Tanzanite uliopo Kimara Kirungule kuna mteja amekuwa akiliibia Shirika letu kwa kutumia umeme ambao haulipii na yeye amechepusha umeme kupitia vishoka,”amesema na kuongeza wateja wote ambao watabainika wameunganisha umeme kinyume na utaratibu hatua za kisheria zitachukuliwa

Bure amesema operesheni inayoendelea sasa inatokana na maelekezo ya Mkurugenzi wa Shirika hilo la TANESCO huku akitumia nafasi hiyo kuwataka wale wote wenye tabia ya kutumia umeme bila kuulipia waaache na wale wenye changamoto wafike katika ofisi zao kutoa taarifa.

Pia amewaomba wananchi wanapobaini baadhi yao kwa wamejiunganishia Umeme kinyume na utaratibu kwa kutumia vishoka kutoa Taarifa TANESCO kupitia namba ambayo unapiga bure ambayo ni 180

Kwa upande wake Mjumbe wa shina namba 10 katika Mtaa wa Amani eneo la Mabibo External Rose Peter amesema TANESCO wamefika katika eneo lake kukagua wale ambao wanaiba umeme kwa kujiunganishia bila utaratibu na kweli wamemkamata watu waliojiunganishia umeme bila utaratibu.

“Kwahiyo kwa wananchi wenzangu nitoe rai tuache tabia ya kuiibia TANESCO umeme .Hii iwe onyo kwa wote ambao wanaiba umeme na ushauri wangu tutumie mita zetu vizuri.”

No comments:

Post a Comment