HABARI PICHA : WATUMISHI OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI WAPATIWA ELIMU YA USALAMA WA MTANDAO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 11, 2026

HABARI PICHA : WATUMISHI OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI WAPATIWA ELIMU YA USALAMA WA MTANDAO

Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Saddy Sevingi akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akifungua mafunzo kuhusu uelewa wa usalama wa kimtandao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Azizi Makaburi akitoa neno la utangulizi wakati wa mafunzo kuhusu uelewa wa usalama wa kimtandao kwa watumishi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Bi. Digna Lyimo akitoa mafunzo kuhusu uelewa wa usalama wa kimtandao kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mtunza Kumbukumbu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Athumani Zunda akiuliza swali kuhusu matumizi ya ngao kwenye mifumo mingine ya Serikali wakati wa mafunzo ya uelewa wa usalama wa kimtandao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Afisa TEHAMA wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Bi. Digna Lyimo (hayupo pichani) wakati akitoa mafunzo kuhusu uelewa wa usalama wa kimtandao kwa watumishi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Usuluhishi wa Kimataifa wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Lydia Thomas akichangia mada wakati wa mafunzo kuhusu uelewa wa usalama wa kimtandao kwa watumishi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment