Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma akizungumza wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kilichojadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12) wakati wa kikao kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026.
 |
| Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Richard Muyungi akichangia hoja wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kilichojadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkatab awa Nairobi (COP 12) wakati wa kikao kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026. |
 |
| Baadhi ya Manaibu Katibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12) wakati wa kikao kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026. |
 |
| Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Nairobi, Dkt. Jaredi Bosile akichangia hoja wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapindiuzi Zanzibar kilichojadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkatab awa Nairobi (COP 12) wakati wa kikao kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026. |
 |
| Kaimu Mkurugenzi Maendeleo Uchumi wa Buluu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Magdalena Ngotolainyo akiwasilisha taarifa kuhusu maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12) wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026. |
 |
| Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu na Watalaamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia mijadala wakati wa kikao hicho kilichojadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkatabawa Nairobi (COP 12). |
 |
| Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia mijadala wakati wa kikao kuhusu maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkatabawa Nairobi (COP 12. |
 |
| Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia mijadala wakati wa kikao kuhusu maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkatabawa Nairobi (COP 12. |
 |
| Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma akiwa katika picha ya pamoja na Watalaamu kutoka Wizara na Taasisi za Umma na Binafsi walioshiriki kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12) katika kikao kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026. |
 |
| Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma akiwa katika picha ya pamoja na watumishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar walioshiriki kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kujadili maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12) katika kikao kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026. |
 |
| Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma akiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Katibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walioshiriki kikao cha kujadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12) katika kikao kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026. |
 |
| Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma (katikati) akifuatilia mijadala wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12) katika kikao kilichofanyika Zanzibar Septemba 16, 2026. |
Kamati ya Makatibu Wakuu na Wataalamu kutoka Wizara na Taasisi za Serikali imehimizwa kuandaa mwelekeo wa kisera na kitaasisi ili kuhakikisha msimamo wa Tanzania unaakisi vipaumbele vya kitaifa kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12).
Hayo yamesemwa Septemba 16, 2026, Unguja Zanzibar na Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu na Watalaam kilichojadili maandalizi ya Tanzania kuelekea Mkutano wa COP 12.
Waziri Hamza amesema dhamana iliyokabidhiwa Tanzania kuelekea mkutano huo ni heshima kubwa kwa taifa hivyo, kunahitaji maandalizi madhubuti, mshikamano na uratibu wa karibu wa taasisi zote za kisekta.
“Mkutano huu una umuhimu mkubwa katika kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambazo zinatilia mkazo maendeleo endelevu, uhifadhi wa mazingira na matumizi bora ya rasilimali za asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho” amesema Hamza.
Aidha Hamza amesema Kamati hiyo inapaswa kuweka msisitizo katika maeneo sita ya kimkakati ambayo ni uimarishaji uchumi wa buluu unaozingatia uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali, kuongeza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika jamii za pwani.
Amebainisha masuala mengine ni pamoja na kuimarisha hatua za kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa bahari, kulinda mifumo ya ikolojia muhimu ikiwemo mikoko, matumbawe na maeneo ya pwani.
Amesema msisitizo huo unatokana na ukweli kuwa rasilimali za bahari zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali, utupaji wa taka bahari na hivyo kuhitajika kuwepo wa sauti ya pamoja kulinda rasilimali hizo.
Ameeleza kuwa mwelekeo m adhubuti kuelekea mkutano huo kutawezesha kuimarisha nafasi ya Tanzania katika uongozi wa uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira ya bahari na ukanda wa pwani katika ukanda wa Magharibi ya Bahari ya Hindi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amesema Kamati ya Makatibu imejipanga vyema katika kuhakikisha maslahi ya Tanzania yanazingatiwa kuelekea Mkutano wa COP 12.
”Tumepanga kuhakikisha Watanzania wote wanapata faida kupitia mkutano wa COP 12 utakofanyika Tanzania....ushauri, maoni na mapendekezo yaliyotolewa na watalaamu yatachakatwa na kujadiliwa kwa kina zaidi” amesema Dkt. Muyungi.
Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi unatekelezwa na Nchi Wanachama 10 ambazo ni Tanzania, Komoro, Kenya, Somalia, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Shelisheli na Ufaransa.
No comments:
Post a Comment