KIRUSWA JIMBO CUP YAINGIA MSIMU WA SITA TIMU 51 KUSHIRIKI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 14, 2026

KIRUSWA JIMBO CUP YAINGIA MSIMU WA SITA TIMU 51 KUSHIRIKI

 


Mashindano  ya Soka ya Kiruswa Jimbo Cup yanayoandaliwa kila mwaka na Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha,Dkt Steven Kiruswa yameingia msimu wa sita na kuendelea kufana kila mwaka na mwaka huu timu 51 zimeshiriki mashindano hayo kutoka katika tarafa nne wa wilaya hiyo yenye wakazi wengi vijana wa jamii ya kifugaji ya Kimasai.

Naibu Waziri huyo alisema hayo baada ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya Kiruswa Jimbo Cup mwaka huu na kusema kuwa mwaka  yatafanikiwa zaidi kwani waandaji wamejipanga kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na  vijana kuchukuliwa kwenda katika ligi za madaraja mengine ya juu timu za huko ili waweze kuiwakilisha vema Longido.

"Sasa mwakani ntakuja kivingine  nataka iwatoe vijana wa kiume na kike wa hapa  Longido kwenda kupata fursa za kimaisha kupitia michezo na kujikita katika michezo zaidi na kuacha mara moja kujikita katika ujambazi, madawa na ulevi"alisema Kiruswa

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Wilaya ya Longido(LDFA) Obeid Mollel amesema Kiruswa Jimbo Cup ni mashindano yanayokuwa mwaka hadi mwaka na vijana wengi wamefanikiwa kusajili katika timu za ngazi mbalimbali Mkoa na ligi daraja la pili na kwanza baada kuonyesha vipaji vyao katika mashindano hayo. 

Mollel alisema timu zote shiriki zimepewa seti moja ya jezi na mpira na washindi watapata zawadi ya fedha taslimu na medali ila mwakani utaratibu utabadilika kwa kuongeza zawadi ya fedha kuwa nono na timu zilizoshika nafasi tatu za juu zitapewa jezi na mpira na sio timu zote kama ilivyokuwa sasa hiyo ni kuongeza ushindani katika soka.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido ,Salumu Kally amesema kuwa Kiruswa Jimbo Cup ni mashindano muhimu katika wilaya yake kwani yanawapa ubize vijana kujikita katika soka na kuacha kujikita katika uhalifu,madawa na ulevi hivyo Mbunge anastahili pongezi na kuungwa mkono kwa hali na mali.

Naye Maenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Papa Nakuta amesema michezo ni ilani ya chama hicho inayosisitiza kuendeleza michezo na anachofanya Kiruswa ni utekelezaji wa ilani ya chama katika kukuza michezo katika Jimbo la Longido na vijana wanafurahia mashindano hayo ambayo yanaonyesha ushindani mkubwa mwaka hadi mwaka.












No comments:

Post a Comment