MKUU WA CHUO IAA AFAFANUA MKAKATI WA KUKUZA WATAALAM SEKTA YA UTALII - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 26, 2026

MKUU WA CHUO IAA AFAFANUA MKAKATI WA KUKUZA WATAALAM SEKTA YA UTALII



Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka, ameeleza kuwa sekta ya utalii ina mchango mkubwa na wa kimkakati katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia ya kisasa katika sekta hiyo, huku msingi wake mkuu unabaki kwenye uzoefu wa kibinadamu, utamaduni, na mila za jamii zetu.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Utalii leo Septemba 25, 2026 katika Hoteli ya Mount Meru hotel jijini Arusha, amesisitiza kuwa IAA itaendelea kuweka jitihada za makusudi ili kuzalisha wataalam na wabobezi bora watakaokidhi mahitaji ya soko la ajira katika sekta hiyo.

​Prof. Sedoyeka amefafanua kuwa siri ya mafanikio ya wanafunzi wa IAA inatokana na mfumo wa mafunzo unaowapa fursa ya kutumia muda mwingi maeneo ya kazi wakishirikiana na wataalam waliobobea huku mfumo huu ukiwawezesha wanafunzi, hasa wanaosomea kozi za utalii, kupata uzoefu wa vitendo na ujuzi wa kutosha kabla hata hawajahitimu masomo yao.

Akifungua Kongamano hilo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili Bw. Nkoba Mabula amesema Sekta ya utalii nchini Tanzania inazidi kuimarika kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa, na msingi wake mkuu unabaki kwenye nafasi ya uzoefu wa kibinadamu, utamaduni, mila na mtindo wa maisha wa jamii zetu.

Bw. Mabula emesema ipo haja ya kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali maeneo ya hifadhi na kutumia teknolojia katika tafiti kutawasaidia watafiti na serikali kupata takwimu sahihi kufanya maamuzi ya kistratejia kwa ajili ya maendeleo endelevu ya utalii nchini Tanzania.

Kongamano la Kimataifa la Utalii Arusha 2026 (AITC) ambalo limeandaliwa na Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA likiwa na kaulimbiu "Ajenda ya Kidijitali na Akili Unde katika Kubuni Upya Utalii", limefanyika kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake mwezi Septemba, 2023.
























No comments:

Post a Comment