MWENGE WA UHURU WAZINDUA BARABARA YA MAILI TANO TABORA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 22, 2026

MWENGE WA UHURU WAZINDUA BARABARA YA MAILI TANO TABORA


Na Mwandishi Wetu - Tabora


Mwenge wa Uhuru 2026 umezindua Barabara ya Maili Tano yenye urefu wa kilomita 2.35, ikiwa ni sehemu ya kilomita 10.7 za barabara za lami zilizojengwa kupitia Mradi wa TACTIC katika Manispaa ya Tabora.

Mradi huo wenye thamani ya Shilingi bilioni 16.46 umekamilika kwa asilimia 100, ukiwa ni miongoni mwa miradi yenye ubora na tija kubwa kwa wananchi kwa kuboresha usafiri, usafirishaji na upatikanaji wa huduma.

Kukamilika kwa mradi huu ni hatua muhimu katika kuboresha miundombinu ya barabara na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Manispaa ya Tabora.

No comments:

Post a Comment