NAIBU KATIBU MKUU AIPONGEZA TANROADS KWA KUCHUKUA HATUA MAPEMA KABLA YA MVUA ZA EL NINO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 24, 2026

NAIBU KATIBU MKUU AIPONGEZA TANROADS KWA KUCHUKUA HATUA MAPEMA KABLA YA MVUA ZA EL NINO


NA MWANDISHI WETU - KILIMANJARO


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, ameipongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuchukua hatua mapema kuimarisha madaraja, makalavati na mifereji kabla ya kuanza kwa mvua za El Niño zinazotarajiwa kuanzia Oktoba 2026.

Dkt. Msonde ametoa pongezi hizo Septemba 23, 2026 wakati akikagua hatua zinazotekelezwa na TANROADS katika Wilaya za Mwanga na Same, ikiwemo kuondoa mchanga na uchafu kwenye njia za maji na kufanya matengenezo katika maeneo yaliyoathirika.

Ameitaka TANROADS kuendelea na ukaguzi na matengenezo ya miundombinu inayohitaji hatua za haraka, huku akiwataka wakandarasi kuongeza kasi ya kazi kabla ya mvua hizo kuanza.

Katika ziara hiyo, Dkt. Msonde amekagua Daraja la Makanya ambalo linafanyiwa matengenezo ya kuimarisha sehemu ya chini na kingo kwa kutumia mawe na zege.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Motta Kyando, amesema ukaguzi umewezesha kubaini mapema maeneo yanayohitaji hatua za haraka.

Amesema TANROADS inaendelea kusafisha Kalavati la Stendi ya Miwa lililojaa mchanga na kuimarisha Daraja la Makanya, pamoja na kusafisha eneo la kuingilia maji ili kuhakikisha maji yanapita kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment