Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, akisalimiana na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mara baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili katika Ofisi hiyo katika ziara ya kikazi leo tarehe 17 Septemba, 2026 Mkoani Geita. Na. Antonia Mbwambo na Helela Lusungu- Nyang’hwale -Geita
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amewataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuhakikisha kuwa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi unazingatia anuai za jamii na mahitaji ya makundi mbalimbali bila ubaguzi, ili kujenga Utumishi wa Umma jumuishi na wenye usawa.
Mhe. Qwaray ametoa kauli hiyo leo, Septemba 17, 2026, wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoani Geita, katika ziara yenye lengo la kutembelea miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto za Watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.
Amesisitiza kuwa uzingatiaji wa anuai za jamii unapaswa kuonekana katika utoaji wa huduma, usimamizi wa watumishi, upangaji wa ajira, mazingira ya kazi na utekelezaji wa stahiki za watumishi.
“Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu wahakikishe kuwa utoaji wa huduma, usimamizi wa Watumishi, upangaji wa ajira, mazingira ya kazi na utekelezaji wa stahiki unazingatia mahitaji na tofauti za makundi mbalimbali ya jamii, bila ubaguzi, ili kujenga Utumishi wa Umma jumuishi na wenye usawa,” amesema Mhe. Qwaray.
Aidha, Mhe. Qwaray amesema Tume ya Utumishi wa Umma inaendelea na ukaguzi wa utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi katika Taasisi za Umma, na kuwataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kushirikiana kikamilifu, kurekebisha mapungufu yatakayobainika na kutekeleza maelekezo ya Tume kwa wakati.
“Kwa ujumla, tunahitaji Utumishi wa Umma unaowajibika, unaozingatia sheria, unaoheshimu haki na kuzingatia anuai za jamii, na unaotoa huduma kwa ufanisi, usawa na kwa wakati,” amesema Mhe. Qwaray.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale, Bi. Kaunga Amani, amemshukuru Mhe. Qwaray kwa kutembelea miradi ya maendeleo na kukutana na watumishi ili kusikiliza changamoto zao. Amesema Halmashauri imepokea maelekezo yaliyotolewa na itaendelea kuyatekeleza ili kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Bi. Husna Toni wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo Mkoani Geita.
Watumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wakimsikiliza Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani GeitaMkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Bi. Grace Kingalame akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) kuzungumza na Watumishi wa Wilaya hiyo Mkoani Geita.
Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa shule wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzungumza na Watumishi katika ziara yake ya kikazi Mkoani Geita

No comments:
Post a Comment