
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda, akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 17,2026 Mtumba jijini Dodoma.
NA OKULY JULIUS, OKULY BLOG, DODOMA
Tume ya Utumishi wa Umma imeonya waajiri wanaokiuka maagizo halali yanayotolewa na Tume kwamba itawapeleka katika mamlaka za juu.
Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa, Septemba 18, 2026, na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda, ambaye amesema waajiri au mamlaka za ajira mbili zimeitwa mbele ya Tume katika kikao chake cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27, kinachotarajiwa kuanza Septemba 21, 2026 hadi Oktoba 16, 2026, jijini Dodoma.
Amesema kitendo hicho, mbali na kuwakwamisha wafanyakazi pekee, bali kinapunguza hata heshima kwa Tume ambayo ni chombo kilichoaminiwa katika kupokea na kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi.
Kipanda amesema wapo waajiri wanaoshindwa kutekeleza maagizo yanayotolewa na Tume wakati wanajua kufanya hivyo ni kuvunja sheria na kutowatendea haki watumishi walio chini yao.
Amesema kitendo hicho, mbali na kuwakwamisha wafanyakazi pekee, bali kinapunguza hata heshima kwa Tume ambayo ni chombo kilichoaminiwa katika kupokea na kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi.
Hayo yanajiri katika kipindi ambacho watumishi wengi wanaopitia kwenye migogoro ya kufukuzwa kazi, kusimamishwa ama kupunguziwa mishahara, wakikata rufaa kwa Tume na kushinda, wamekuwa hawatendewi kama ambavyo Tume inaagiza.
“Hizo mamlaka mbili tumewaita wahusika wenyewe, siyo wawakilishi wao, na wasipokuja tunapeleka malalamiko haya mezani kwa Katibu Mkuu Kiongozi kwa hatua zaidi za kinidhamu,” amesema Kipanda.
Katika kikao kitakachokutana hivi karibuni kwa mara ya kwanza katika Jengo la Tume lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Katibu amesema wataanza kwa kutoa mafunzo na kisha kupitia rufaa za watumishi ambazo, hata hivyo, hakutaja idadi yake. Kwa upande wa warufani, amesema 16 kati yao watafika mbele ya Baraza hilo kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu mashauri yao.
Amesema mbali na mkutano huo, Tume inaendelea na zoezi la ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa utumishi wa umma, ambalo lilizinduliwa na Waziri mwenye dhamana, Ridhiwan Kikwete, Agosti 10, 2026, na hadi sasa wamefikia taasisi 97 kati ya 300 wanazozilenga kabla ya Desemba 12, 2026.
Akizungumzia ukaguzi huo, Naibu Katibu anayeshughulikia uzingatiaji wa sheria, Celina Maongezi, amesema suala la utawala, usimamizi na usalama mahala pa kazi ni miongoni mwa maeneo yanayojitokeza zaidi katika taasisi zilizokaguliwa.
Maongezi ametaja eneo lingine ambalo linaonyesha kuwa na shida kuwa ni upande wa mafunzo kwa watumishi, ambayo anasema yanalalamikiwa na baadhi ya watumishi.
Naibu Katibu wa Tume, John Mbisso, amewataka watumishi wenye changamoto ambao wangependa kuwasilisha malalamiko yao watambue kuwa hivi sasa ofisi zinazotumika ni Mtumba na siyo UDOM tena.
Mbisso amesema majengo ya Mtumba yako vizuri, hata kwa kukaa faragha kwa ajili ya kuzungumzia jambo lolote na mtumishi, huku likiwa limechukua watu wote kutoka Tume, ambapo mtu anaweza kukutana na kitengo chochote kwa wakati mmoja.

No comments:
Post a Comment