UDOM YAKABIDHI AI ULTRASOUND KWA VITUO 32 DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 15, 2026

UDOM YAKABIDHI AI ULTRASOUND KWA VITUO 32 DODOMA

Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Tanzania imeendelea kupiga hatua katika matumizi ya Akili Unde ambapo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimekabidhi vifaa vya kisasa vya upimaji wa mama wajawazito, vinavyotumia teknolojia ya AI Ultrasound kwa vituo 32 vya kutolea huduma za afya katika mkoa wa Dodoma vyenye thamani ya shilingi milioni 352.


Hatua hiyo imefanyika leo Spetemba 15,2026 katika kituo cha afya Mkonze Jijini Dodoma, kupitia Mradi wa SAFARI, unaolenga kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto kwa kutumia teknolojia na kuongeza uwezo wa wahudumu wa afya katika kufanya uchunguzi wa wajawazito.


Akizungumzia hatua hiyo Mkuu wa mkoa huo Rosemary Senyamule amesema hatua hiyo itaongeza uwezo wa vituo hivyo vya afya kutoa huduma bora za uchunguzi bila mgonjwa kusafiri umbali mrefu kwaajili ya uchunguzi wa afya ya mama na mtoto.

"Vifaa hivi vitatumika kama chombo cha awali katika vituo vyetu vya afya, mama mjamzito atakayegundulika kuwa na viashiria vya changamoto au matatizo yoyote wakati wa uchunguzi huo atapewa rufaa haraka kwenda vituo vya ngazi ya juu zenye wataalamu na wabobezi zaidi vya Ultra sound kwaajili ya uchunguzi wa kina na kwaajili ya matibabu,"amesema.


Katika hatua nyingine RC Senyamule amewaekeza Waganga wa Halmashauri na watumishi wa vituo vya afya watakao kabidhiwa vifaa hivyo kuhakikisha wanatunza vifaa hivyo na kuvitumia ipasavyo ili viendelee kusaidia huduma iliyokusudiwa.


Kwa upande wake Naibu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Nasoro Mzee ametoa rai kwa Wakuu wa Wilaya watakao kabidhiwa vifaa hivyo kuhakikisha vinatumika ipasavyo na sio kwenda kuvifungia stoo.


Naye Mkurugenzi wa Shahda ya Uzamili kutoka UDOM Prof. Josephat Kiligiti amesema mradi huo ni kujifunza namna teknolojia ya Akili Unde inaweza kuunganishwa katika ufanisi wa huduma za kawaida za afya ya mama na mtoto katika ngazi za msingi.


"Ni muhimu kutambua kwamba changamoto ya upungufu wa wataalamu wa ultra sound sio tatizo la Dodoma pekee bali ni tatizo la kitaifa na hata kimataifa katika nchi nyingi zinazoendelea, teknolojia hii inaweza kuziba pengo hilo,"amesema.


Awali mtafiti mkuu wa mradi huo Dkt. Leonard Katalambula emesisitiza kuwa teknolojia hiyo haichukui nafasi ya mtoa huduma wala mtaalamu bali ni chombo kinachomsaidia mtoa huduma kufanya uchunguzi na kufanya maamuzi kwa wakati kwa kuzingatia taratibu za kitaalamu.









No comments:

Post a Comment