Katika hatua hiyo, wadau wa elimu wamekutana jijini Arusha katika kikao kazi kuanzia Septemba 22 hadi 26, 2026, kwa ajili ya kutathmini utekelezaji wa shughuli za Partnership Compact katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27, kubaini hatua zilizofikiwa na kutathmini mchango wa juhudi hizo katika kutekeleza vipaumbele vya Sera ya Elimu na Mafunzo nchini.
Mkutano huo umesisitiza umuhimu wa kuongeza mikakati ya uhamasishaji wa rasilimali ili kuiwezesha Serikali kutekeleza kwa ufanisi mpango wa elimu ya lazima ifikapo mwaka 2028, ambapo makundi rika mawili ya wanafunzi yanatarajiwa kuingia Kidato cha Kwanza.
Kupitia Partnership Compact, Serikali na wadau wa elimu wanaendelea kuunganisha nguvu, utaalamu na rasilimali katika kuunga mkono vipaumbele vya elimu nchini. Ushirikiano huo unalenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya elimu na kuhakikisha sekta inaendelea kuimarika na kutoa fursa za elimu kwa watoto na vijana nchini.






No comments:
Post a Comment