WANANCHI 11,772 BAHI WAIPONGEZA RUWASA WAKIFURAHIA HUDUMA YA MAJI SAFI YA BOMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 23, 2026

WANANCHI 11,772 BAHI WAIPONGEZA RUWASA WAKIFURAHIA HUDUMA YA MAJI SAFI YA BOMBA


Wananchi wa Kata ya Ibihwa, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, wameeleza kufurahishwa na upatikanaji wa huduma ya maji safi, salama na ya uhakika kupitia miradi inayotekelezwa na RUWASA.

Wakizungumza wakati wa ziara ya kutembelea na kuona hali ya upatikanaji wa maji iliyoratibiwa na Kitengo Cha Uhusiano na Masoko cha RUWASA Septemba 22, 2026, wananchi hao wamesema huduma hiyo imeleta mabadiliko makubwa katika maisha yao, ikiwemo kupunguza umbali na gharama za kutafuta maji.

Alio Nyatoto, mkazi wa eneo hilo, alisema hali ya maji kwa sasa ni nzuri tofauti na zamani ambapo walitembea takribani dakika 15 kutafuta maji kwenye makorongo. Justina Clement amesema awali walinunua maji kwa shilingi 300 hadi 500 kwa ndoo, lakini sasa wanapata maji safi na ya uhakika kwa shilingi 50 kwa ndoo.

Naye Daudi Spiru alisema mradi huo umeleta manufaa makubwa kwa wananchi waliokuwa wakitegemea maji ya mtoni ambayo yalikuwa machafu na kupungua wakati wa kiangazi. Dorothea Sanguti amesema, “Zamani tulichota maji ya kwenye makorongo, shule na kwa mapadre. Hali ya sasa ni tofauti, maji ni mengi na masafi.”

Kwa upande wake, Katibu wa CBWSO ya Umonga, Pudensiana Pancras, alisema CBWSO hiyo ilianzishwa tarehe 28 Juni 2024 na inahudumia kata nne ambazo ni Ibihwa, Bahi, Ilindi na Mpamatwa zenye jumla ya vijiji nane.

Alisema CBWSO hiyo ina vituo 45 vya kuchotea maji na miunganisho 120 ya majumbani, huku mradi ukinufaisha wananchi 11,772. 
Kisima hicho kilichochozinduliwa mwezi Agosti 2024 kinazalisha lita 36,000 za maji kwa saa na kutoa huduma Kwa Wananchi pamoja maeneo ya Umma kama Shule na vituo vya afya .

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Bahi Mhandisi Hopeness Liundi alisema hali ya upatikanaji wa Maji umefikia vijiji 53 kati ya Vijiji 59 vilivyopo katika Wilaya hiyo sawa na asilimia 89 huku vijiji viwili vikiwa kwenye mpango wa uendelezaji katika mpango wa 1575 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Mhandisi Hopeness aliongeza kuwa upatikanaji wa maji katika Mazingira ya karibu imepunguza umbali na gharama za maisha Kwa wananchi kutafuta maji umbali mrefu.

No comments:

Post a Comment