ASAS AENDELEZA UTAMADUNI WA KUTEMBELEA WANANCHI, AWAFIKIA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI WERU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 20, 2026

ASAS AENDELEZA UTAMADUNI WA KUTEMBELEA WANANCHI, AWAFIKIA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI WERU


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MCC), Salim Abri Asas, ametembelea na kuwasalimia wanafunzi wa Shule ya Msingi Weru, iliyopo katika Jimbo la Kalenga, Wilaya ya Iringa Vijijini.

Ziara hiyo imelenga kuimarisha uhusiano wa karibu na jamii, pamoja na kujionea mazingira ya wanafunzi wanapotekeleza shughuli zao za kila siku za kujifunza.

Kupitia ziara hiyo, Asas ameonesha umuhimu wa viongozi kuendelea kuwa karibu na wananchi, hususan watoto na vijana, ambao ni msingi wa maendeleo ya taifa.

Mawasiliano ya karibu kati ya viongozi, wanafunzi na wadau wa maendeleo ni fursa muhimu ya kutambua mahitaji ya jamii na kutafuta njia za kuboresha mazingira ya elimu na ustawi wa watoto.





No comments:

Post a Comment