DKT. HOMERA AKUTANA NA WATENDAJI WA KAMPUNI YA VIVO ENERGY - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 22, 2026

DKT. HOMERA AKUTANA NA WATENDAJI WA KAMPUNI YA VIVO ENERGY


Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam.


Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, leo Oktoba 22, 2026, amekutana na watendaji wa Kampuni ya Vivo Energy inayojishughulisha na usambazaji wa mafuta na vilainishi katika nchi mbalimbali duniani, ambapo wamejadili masuala ya uwekezaji, ikiwemo nia ya kampuni hiyo kupanua shughuli zake nchini Tanzania.


Katika mazungumzo hayo, Mtendaji wa Kampuni ya Vivo Energy nchini Tanzania, Mohamed Bougriba, amemweleza Dkt. Homera kuwa kampuni hiyo ina nia ya kupanua wigo wa uwekezaji wake kwa kujikita katika sekta nyingine, zikiwemo maji, madini na nishati safi ya kupikia.

 Dkt. Homera ameipongeza kampuni hiyo kwa shughuli zake za usambazaji wa mafuta na vilainishi pamoja na kuonesha nia ya kuwekeza katika nishati safi ya kupikia, akieleza kuwa uwekezaji huo utachangia juhudi za Serikali za kufikia lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

No comments:

Post a Comment