Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mark Njera, Oktoba 7, 2026, amezindua kampeni ya “Ongea na Kamanda” kwa kufanya mkutano na wananchi wa Kijiji cha Mkwengwa, Kata ya Nyamunga, Wilaya ya Kinesi.
Katika mkutano huo, Kamanda Njera amewataka wazazi na walezi kuzingatia malezi bora ya watoto ili kuwajenga katika maadili mema na kuwalinda dhidi ya vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha na usalama wao.
Akizungumza na wananchi, Kamanda Njera amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao, kuwafuatilia kwa ukaribu na kuwapa malezi yanayozingatia maadili, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kujenga jamii yenye nidhamu na maadili mema.
Amesema ushirikiano kati ya Polisi na wananchi ni muhimu katika kuimarisha usalama wa jamii, huku akiwataka wananchi kutumia kampeni hiyo kutoa taarifa na changamoto zinazowakabili.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, pamoja na kutoa nafasi kwa wananchi kueleza changamoto zao na kujenga mazingira salama na yenye utulivu.

No comments:
Post a Comment