Afisa Mnadhimu Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Desdery Rugimbana amewataka askari wa usalama barabara kuchukua hatua za kisheria kwa baadhi ya madereva wazembe wasiozingatia Sheria za Usalama barabarani na kusababisha ajali zinazopelekea vifo na majeruhi.
ACP Rugimbana, ametoa kauli hiyo Oktoba 09, 2026 eneo la Vigwaza Mkoani Pwani wakati akifanya ziara ya kukakugua utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani na kutoa elimu Kwa madereva pamoja na askari hao ili KUDHIBITI ajali zisizo tarajiwa.
Vilevile Rugimbana, amesisitiza askari wa usalama barabara kutoa huduma bora kwa jamii na kuhakikisha madereva wanaokiuka Sheria za usalama barabara wanachukuliwa hatua stahiki ikiwemo kutozwa faini na kufikishwa mahakamani.
Katika hatua nyingine Rugimba amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi wanapoona ukiukwaji wa Sheria za usalama barabarani ili kudhibi matukuio ya ajali za barabarani yanayoweza kuleta taharuki katika Jamii.







No comments:
Post a Comment