
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kadogosa, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Nyongo, leo Oktoba 9, 2026.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kadogosa ameeleza mipango ya Wizara ya Ujenzi katika kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha nchini, pamoja na mikakati ya kupunguza msongamano wa magari mkoani humo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Nyongo, ameiomba Wizara ya Ujenzi kuangalia uwezekano wa kukarabati barabara ya Nyamwage–Utete yenye urefu wa kilometa 33.4 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii na kuchochea shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.
Aidha, ameomba barabara ya Old Morogoro kukarabatiwa ili kuwezesha malori kutumia njia hiyo na hivyo kupunguza msongamano wa magari katika barabara ya Dar es Salaam–Morogoro.






No comments:
Post a Comment