Na Mwandishi Wetu - Katavi
Waziri wa Madini Mhe.Anthony ameelekeza kufutwa kwa leseni kubwa saba ikiwemo Leseni ya Uchimbaji wa Kati (ML) na Leseni za Utafiti (PL) mkoani Katavi.
Maelekezo hayo, yametolewa leo Novemba 13, 2026 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akigawa leseni kwa vikundi tisa (9) vya wachimbaji wadogo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Program ya (MBT), ikiwa ni mpango kufuta leseni ambazo hazifanyiwi kazi na kutolewa kwa Vijana, Wanawake na watu wenye uhitaji maalum.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa leseni , Waziri Mavunde amesema kuwa, utoaji wa leseni ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
“Wakati wa ziara ya Mh. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba mliwasilisha changamoto ya upatikanaji wa maeneo ya kuchimba na Mh. Waziri Mkuu aliielekeza Wizara kuchukua hatua ili wale wote wasioendeleza maeneo yao kurejeshwa serikalini na kugawiwa kwa wachimbaji wadogo”Amesema Mavunde
Waziri Mavunde ameeleza kuwa, pamoja na wachimbaji wadogo kupatiwa fursa hiyo, pia wawekezaji wakubwa wenye nia ya kuendeleza maeneo ya uchimbaji ndani ya katavi pia watatizamwa.
Waziri Mavunde ameeleza kuwa, mkoa wa Katavi ni mkoa wenye madini mbalimbali hivyo lengo la serikali ni kuondoa utaratibu wa watu wachache kumiliki eneo kubwa leseni bila kuendeleza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda , Mhe.Jamila Kimaro ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuwapatia leseni vijana , wakina mama na watu wenye uhitaji maalum jambo litakalosaidia katika kujiendeleza na kujiunua kiuchumi.
Pia, amemshukuru Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya bilioni 296 katika wilaya ya Mpanda.
Hafla hiyo ya utoaji wa leseni , imeudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa CCM Mkoa wa Katavi na Wilaya,wataalam kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya.






No comments:
Post a Comment