DCEA YANG'ARA TUZO ZA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 27, 2026

DCEA YANG'ARA TUZO ZA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za serikali zinazojitegemea kwenye Tuzo za Ubora wa Uandaaji na Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Akizungumza leo Novemba 26, 2026 Jijini Dar es Salaam baada ya kupokea tuzo hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema ushindi huo ni chachu kwa mamlaka hiyo na uthibitisho wa kuzingatia vigezo vya kimataifa katika uandaaji wa taarifa za fedha, uwazi na matumizi bora ya fedha za umma.

Lyimo ameishukuru NBAA kwa kutambua mchango wa mamlaka hiyo katika kuimarisha mifumo ya uandaaji wa hesabu kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, akisema tuzo hiyo inaonesha juhudi zinazofanywa na watumishi katika kuhakikisha uwajibikaji na ufanisi wa matumizi ya rasilimali za serikali.

Aidha, amewapongeza watumishi wa DCEA, hususan Kitengo cha Fedha na Uhasibu pamoja na Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, kwa mchango wao katika kufanikisha mafanikio hayo kupitia usimamizi, ukaguzi na uandaaji bora wa taarifa za fedha.

Amesema DCEA itaendelea kudumisha viwango hivyo vya kimataifa kwa kuhakikisha inatumia fedha za umma kwa ufanisi na weledi, sambamba na kuimarisha utekelezaji wa majukumu yake ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini.

Amesisitiza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji, uwazi na matumizi sahihi ya rasilimali za serikali ili kuongeza ufanisi katika utendaji wake.

No comments:

Post a Comment