SERIKALI YAENDELEA KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU NCHINI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 28, 2026

SERIKALI YAENDELEA KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU NCHINI.


Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Musa Omar (Mb), akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Henry Chalu wakati wakisubiri kuanza maandamo ya kitaaluma katika Mahafali ya 52 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Musa Omar (Mb), akizungumza wakati wa Mahafali ya 52 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Musa Omar (Mb), akiwatunuku shahada mbalimbali wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wakati wa Mahafali ya 52 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.


(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, WF – Dar Es Salaam)


Na. Josephine Majura na Asia Singano, WF - Dar Es Salaam


Serikali inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kukuza sekta ya elimu ambapo ukuaji huu unajidhihirisha kwenye maeneo mbalimbali ya sekta, hususani jitihada zinazoendelea kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), Mahafali ya 52 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), tarehe 28 Novemba 2026 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dimond Jublee jijini Dar Es Salaam, alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo.

Alisema Serikali inaendelea kuwekeza na kuhakikisha kuwa suala ya kupata elimu yenye ubora na inayozingatia usawa wa jinsia linapewa kipaumbele ili kujenga taifa lililoelimika na lenye watu wenye elimu yanye ubora inayohitajika katika dunia ya leo

‘’Katika hili kwa upande wa elimu ya juu tumeendelea kutekeleza miradi mbalimbali moja wapo ni mradi ambao unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia ambao kwa ufupi unaitwa HEET, lakini mradi wa elimu ya juu wa mageuzi ya kiuchumi mradi huu uliundwa umeundwa ili kufufua na kupanua uwezo wa vyuo vikuu kuchangia katika maeneo muhimu ya uvumbuzi, maendeleo ya kiuchumi’’ alisema Mhe. Balozi Omar (Mb).

Alisema Serikali imeendelea kuongeza bajeti yake katika sekta ya elimu kila mwaka ili kuwezesha wanafunzi kujikimu wakati wa masomo na kupata elimu bora inayoendana na mazingira ya sasa.

‘’Ongezeko la asilimia 85 kwa upande wa mikopo na ruzuku ya elimu ya juu kwa miaka mitano iliyopita ambapo tumetoka shilingi bilioni 570 mwaka 2021/2022 kufikia Shilingi trilioni 1.06 katika mwaka wa masomo 2026/2027’’ alisema Mhe. Balozi Omar (Mb).

Akizungumzia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mhe. Balozi Omar, alisema Dira 2050 inaitambua sekta binafsi kama injini kuu ya ukuaji na ajira, na inasisitiza ujasiriamali wa wazawa na kurasimisha biashara ndogo na za kati, ikilenga Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu bora barani Afrika katika urahisi wa kufanya biashara huku akiwasisitiza wahitimu hao kuwa sehemu ya utekelezaji wake kwakuwa ndio kizazi cha Dira hiyo.

Alisema huduma za Fedha ni mojawapo ya sekta tisa za kimkakati za Dira, hivyo wahitimu wa IFM mko katikati ya safari hii. Dira inakusudia kuimarisha masoko ya mitaji, kupanua ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), na kupanua huduma jumuishi za kifedha kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu’’ alisema Mhe. Balozi Omar (Mb).

Awali akizungumza wakati wa Kumkaribisha Mgeni Rasmi, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Prof. Emanuel Mjema, alisema chuo hicho kinaendelea kusogeza huduma karibu na wananchi ili kuhakikisha elimu inawafikia wanafunzi wengi kutoka maeneo mbalimbali.

‘’ Kwa sasa hivi Chuo chetu kina Kampasi ya Dar Es Salaam ambayo ndio Kampasi Kuu, tuna Kampasi Dodoma, Mwanza, Simiyu Geita pamoja na Zanzibar kama alivyoeleza Kaimu Mkuu wa Chuo’’Alisema Prof. Mjema.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Prof. Henry Chalu, alisema chuo hicho kimekuwa kikiongeza idadi wa wanafunzi kutokana ubora wa elimu inayotolewa na wataalam wa chuo hicho.

‘’Kwa mwaka wa masomo ambao ndio umekamilishwa kwa wanafunzi waliomaliza idadi ya wanafunzi imeongezeka kwa asilimia 11.9 ikilinganishwa na mwaka wa masomo uliopita yaani 2024/2025’’ alisema Pro. Chalu.

Katika Mahafali hayo ya 52 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), yenye wahitimu takribani , Mhe. Balozi Omar kuwatunuku vyeti na zawadi wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Kampasi ya Dar es Salaam na Kampasi ya Zanzibar, kwa mwaka wa masomo 2025/2026, katika ngazi za Astashahada, Stashahada, Shahada ya Kwanza, Stashahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamili, ninyi nyote waliokidhi vigezo vya kufuzu.


Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Henry Chalu, akizungumza wakati wa Mahafali ya 52 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Musa Omar (Mb), akiondoka katika ukumbi wa Daimond Jubilee baada ya kumaliza zoezi la kuwatunuku wahitimu wa shahada mbalimbali wakati wa Mahafali ya 52 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Musa Omar (Mb), akitoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika ngazi mbalimbali wakati Mahafali ya 52 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.



Mweneyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa mahafali ya 52 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment