WAFANYABIASHARA KARIAKOO, MACHINGA COMPLEX WAHIMIZWA KUWEKA AKIBA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 14, 2026

WAFANYABIASHARA KARIAKOO, MACHINGA COMPLEX WAHIMIZWA KUWEKA AKIBA.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewashauri wafanyabiashra kutumia vema mapato wanayo yayapata na kuhakikisha kuwa wanaweka akiba katika biashara zao jambo ili kukuza kipato chao, kufanya maendeleo na biashara zao kuwa endelevu zaidi.

Mhe. Mpogolo ameyasema hayo Novemba 13 2026 jijini Dar es Salaam, wakati akihitimisha bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo na kuwashirikisha wafanyabiashara wa Soko la Machinga, kuwa japo biashara hizo ni zao wanao wajibu wa kupata faida na kujilipa mishahara.

Ameupongeza uongozi wa Shirika hilo kwa kuandaa bonanza na kuongeza kuwa wafanyabiashara hao wanapaswa kutumia fursa, zinazotokana na bonanza hilo kukuza ushirikiano, urafiki na fursa za biashara baina yao kwa kuwa Serikali imeshaweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujenga masoko ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanafanya biashara katika mazingira rafiki, yenye utu na yanayojali staha kwa wafanyabiashara na kuongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia ameagiza kujengwa na kukamilika kwa Soko la wamachinga ndani ya miezi sita na kubainisha kuwa soko hilo litajengwa eneo la Kigogo Sambusa.

Kwa upande wke Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Ashraph Abdulkarim amesema bonanza hilo limelenga kukuza urafiki, umoja na mshikamano baina ya watumishi, wafanyabiashara wa Kariakoo, na Soko la Machinga Complex.

Ameongeza pia michezo ni sehemu ya kukuza upendo, mshikamano, amani na pia kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuepuka tabia bwete kwa kufanya mazoezi na ameahidi mabonanza kama hayo kuwa endelevu.

Katika bonanza hilo timu ya mpira wa miguu na mpira pete ya Machinga Complex zilishinda na kupata medali, kombe na fedha huku Shirika la Masoko ya Kariakoo likipata medali katika michezo ya mpira wa miguu na pete na pia kupata kombe kwenye mchezo wa kuvuta Kamba.

No comments:

Post a Comment